ILI MUZIKI WETU UWEZE KWENDA KIMATAIFA NI LAZIMA TUBADILIKE, SAPOTI YAKO PIA MUHIMU

Eneo la Kunduchi Wet n' Wild linavyoonekana kwa nje
Mara tukaingia ndani, hebu cheki maujanja
Mara mfanyakazi mwenzangu Sista Doi alianza kuweka mapozi pembeni swiming pool. Kwa ishu zaidi mcheki kupitia Blog yake www. Sisterdoi.blogspot.com
Kabla ya yote tulianza kuangusha moja moja kwenye vinywaji, kama tunavyoonekana mimi na Shaluwa a.k.a Jopasha

Kilichofuata ni msosi. Ebwana ulikuwa wa ukweli.
Kisha tukaanza kujiachia majini kwenye swiming, full kuogelea
Mimi na mama wa Mpaka Home, Imelda tukishindana kupiga maji
Nilipotoka nje ya maji kupumzika nikagonga pozi moja la ukweli na Cralence a.k.a Tusichoshane, Sidanganyiki
Kutoka kushoto: Mussa Mateja, Tusichoshane na mimi tukipumzika
Kushoto: Tusichoshane, Walter a.k.a Mcharuko na mimi tukijiandaa kurudi home baada ya kazi ngumu ya kustarehe Wet n' Wild.


Mwishoni mwa wiki iliyopita mimi na wafanyakazi wenzagu wa Kampuni ya Global Publishers tulipata fulsa ya kwenda kupumzika pande za Kunduchi Wet n' Wild ili kupunguza uchovu mara baada ya kazi ngumu ya kuandaa magazeti yetu. Huo ni utaratibu uliowekwa na uongozi wa kampuni yetu ambapo kila mwaka tunatoka na kwenda kupumzika sehemu tulivu kwa ajili ya kupunguza 'Ma-folda yenye Virus' vichwani mwetu kutokana na kazi ngumu tunayoifanya.

Read More......
Tuesday, October 27, 2009 Posted in | | 0 Comments »

MB katika pozi
Mke mtarajiwa wa MB akiwa na marehemu mtoto wao, Suu
MB akiwa na mwanawe wa kwanza,
MB akiwa na Suu, mwanawe wa pili aliyefariki dunia hivi karibuni

Baada ya kuondokewa na mwanawe mpendwa, Suu miezi kadhaa iliyopita na kufanikiwa kumaliza arobaini salama, mwana Bongo Flava Mohamed Mbwana a.k.a MB Dog amesema na ebwana daah kwamba kitakachofuata ni kumchukua jumla msichana aliyezaa naye mtoto huyo na kupiga naye maisha kama mke na mume.
MB alisema kwamba kabla ya zoezi hilo anafanya mishemishe za kukamilisha video za nyimbo mpya mbili kisha kumsogeza ndani maiwaifu wake huyo mtarajiwa kwa ndoa halali ambayo itawapa shavu baadhi ya mastaa wa Kibongo.
"Hakuna kinachoshindikana chini ya jua, hivi sasa nipo kwenye mishemishe za kugonga video zetu mbili, moja ya kwangu nimewashirikisha Yakuza Mobb, nyingine ya kwao wamenipa shavu. Ngoma hizo ambazo bado hatujazipa majina tulizifanya Nairobi, Kenya. Baada ya hapo nitamsogeza waifu ndani tuendeleze harakati za kupambana na maisha," alisema Dog ambaye hivi sasa anafanya vyema na ngoma yake, Saga Plasher.

Read More......
Posted in | | 0 Comments »

Leo J'5 dada yangu wa ukweli, Huruma Bujiku a.k.a Mama Nyaku a.k.a Mama Bujiku a.k.a ........Mungu amemjalia katimiza umri wa miaka ......(siri yake). Katika kusheherekea tukio hilo muhimu kwake ameamua kuwapa shavu wafanyakazi wenzake wa Kampuni ya Global Publishers kwa kuwalisha vipande vya keki maalum nikiwemo mimi (si unanicheki). Tunampongeza kwa kuongeza mwaka mwingine kunako dunia hii yenye kila aina ya vurugumechi, tunamuomba Mungu ampe maisha marefu zaidi. Big Sista Huruma. Happy Birthday tuyuuuuuuuuuu!!!!!.

Read More......
Tuesday, October 20, 2009 Posted in | | 0 Comments »

Pichani Mhe. Zitto Kabwe (katikati) akiwa katika pozi na baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni ya Global Publishers nikiwemo mimi (mwenye kofia nyeupe) na Mkurugenzi wetu, Eric Shigongo (kulia kwa Zitto), alipotutembelea leo.
Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Mhe. Zitto Kabwe leo alitutembelea ofisini na kutupa moyo kwa kazi ngumu tunayoifanya na kujibu maswali machache tuliyomuuliza. Big Up Zitto, unakaribishwa tena siku nyingine.

Read More......
Friday, October 16, 2009 Posted in | | 0 Comments »

Leo ni siku ya kumbukumbu ya Baba wa Taifa, mimi na staff wenzangu tunaungana na Wabongo wote katika siku hii muhimu, ambayo hufanyika mara moja kila mwaka tarehe 14/10

Kama unavyotuona, wengi wamevaa t-shirt zenye picha ya Mwalimu na maandishi Thumbs Up for Mwalimu ambayo mimi na mdogo wangu Walter tulishirikiana kui-designer.

Read More......
Wednesday, October 14, 2009 Posted in | | 0 Comments »

Karibu asilimia 80 ya mashabiki waliyofurika katika ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar walikuwa wakimpa shavu Pascal
Pascal akikabidhiwa mfano wa hundi yenye thamani ya Em 24 kutoka kwa wadhamini wa mpambano huo
Madam Ritta: BSS tunahitaji kijana kama wewe, hongera sana

Hatimaye kijana Pascal Casian kutoka pande za Rock City (Mwanza) jana usiku ameibuka na ushindi kupitia mpambano wa kufatufa vipaji 'BSS' na kuondoka na mkwanja wa kutosha, yaani Em 24. Pascal alifuatiwa na Peter Msechu kutoka KG yaani Kigoma aliyeshika nafasi ya 2, huku nafasi ya tatu ikienda kwa Kelvin Mbati. Mshindi wa nne ni Jackson George na aliyeambulia tano bora ni Beatrice William. Big Up kwa waandaaji, Benchmark Production, changamoto iliyopo mbele yenu ni kumfanya kijana Pascal asimame kupitia game ya muziki wake.

Read More......
Posted in | | 0 Comments »

A.Y: Nimejifuunza mengi MTV Africa Music Awards, nitafika tu.
M.I kutoka Nigeria aliyechukua Tuzo zote mbili
Shaa

Kama ulikuwa haumfahamu mchizi aliyelamba tuzo zilizokuwa zinawaniwa na A.Y pamoja na Shaa kupitia MTV Africa Music Awards zilizotolewa Nairobi, Kenya mwishoni mwa wiki iliyopita ni huyo M.I kutoka pande za Nigeria. Tuzo aliyokuwa anawania na Shaa ni ya Msanii bora anayechipukia, huku ya A.Y ikiwa ni ya Mwana Hip Hop bora. Ishu kubwa ni kura chache zilizowaangusha wasanii wetu wa Kibongo.

Read More......
Posted in | | 0 Comments »

MERCEDES BENZ 230E 4CYLINDER 5SPEED INAUZWA IKIWA KATIKA HALI NZURI, BEI MIL.6. KWA MAWASILIANO CHEKI NA SISI KUPITIA SIMU NAMBA 0784 252522, 0754 252522, 0655252522.

Read More......
Tuesday, October 6, 2009 Posted in | | 0 Comments »