Msanii Langa Kileo amefunguka kwamba baada ya kuzama katika utumiaji wa dawa za kulevya na kuamua kuachana nazo hivi karibuni anataka jamii imtambue kama Rais wa Mateja ambaye atakuwa mfano mzuri kwa wenzake ambao bado wanaendelea kutumia.
Langa alisema kuwa miaka kadhaa iliyopita alijikuta akizama katika utumiaji wa dawa hizo baada ya kugongea fegi iliyokuwa imemiksiwa na drugs kutoka kwa mshikaji wake na alipovuta tayari stimu zikawa zimemuingia na kumfanya aendelee kubembea hadi hivi karibuni alipoamua kujivua gamba la uteja.
"Ilifikia wakati nikahama nyumbani japo kimaisha mzee yuko poa na kwenda kuishi kwenye mageto ya washikaji tukipiga dili za kuvuta unga na kuiba. Nilikonda na kupoteza nguvu kabisa, ilibaki hatua ya mwisho kwenda kupiga debe kwenye vituo vya daladala, lakini nashukuru Mungu nimefanikiwa kuchomoka huko.
"Wengi ambao bado wanaendelea kutumia watajiuliza nimewezaje kuachana, wapo watakaonionea wivu kwa hilo kwasababau ni kazi ngumu kidogo kujiondoa katika kundi hilo, ila nitaendelea kufanya kampeni za kuwahamasisha wengine pia kuacha kwani inawezekana," alisema.
Ebwanadaah inampongeza Langa kwa ujasiri huo na kumuombea kwa Mungu afya yake izidi kuwa poa kwani jamii bado inahitaji kupata elimu kupitia ngoma zake.
Saturday, July 16, 2011
Posted in | |
0 Comments »
One Responses to "LANGA SASA NI RAIS WA MATEJA"