Temba na Chegge
Kundi la TMK Wanaume Family a.k.a Watoto wa Kiume watashuka pande za Mbezi Luis, Dar es Salaam kwa kazi mbili za nguvu, kuitambulisha ngoma na muvi yao yenye jina ka Kichwa kinauma pamoja na kumuweka mbele ya hadhara dogo anayefanya vizuri sasa na ngoma yenye jina la Nakusemea, anaitwa Aslay Isiaka.
Mpango mzima wa burudani hiyo utachukua nafasi Jumamosi ya Machi 3, mwaka huu ndani ya Ukumbi wa times Square uliyopo pande hizo, huku wakipewa sapo na wasanii wengine kibao nikiwemo mimi George MC na ngoma yangu Narudi Nyumbani, bila kumsahau 'Shostito' wangu, Zuhura a.k.a Limupenzi ambaye anafanya vyema na ngoma yenye jina la Ukubwa jalala.
Pia wasanii wapya wanaoibuka pande hizo watapata nafasi ya kuonesha vipaji vyao vya kuimba na mshindi mmoja atakula shavu la kurekodi ndani ya studio za Poteza Records zilizomtoa Dogo Aslay. Kiingilio katika shoo hiyo kitakuwa ni shilingi 3000 kwa kila mtu. Njoo wewe na yule mpenda burudani. Mbezi sasa mmekumbukwa.

Tuesday, February 7, 2012
Posted in | |
0 Comments »
One Responses to "TMK FAMILY KUSHUKA MBEZI NA ASLAY"