ILI MUZIKI WETU UWEZE KWENDA KIMATAIFA NI LAZIMA TUBADILIKE, SAPOTI YAKO PIA MUHIMU

Mchizi kutoka Ujerumani alisimamia zoezi zima la picha

Muongozaji wa mzigo huo pia hakubaki nyuma. Picha zikiendelea kuchukuliwa
Madansa wakipiga ishu

Ommy G na mimi pia tulikuwepo
TDX, Mimi, Sule Inc
TDX, Ommy G na mimi
Gheto King, Ommy G na Mimi

Katikati ya wiki iliyopita, mchizi wangu Saimon John, Gheto King a.k.a Saidwog aligonga video ya ngoma yake mpya, Saidwog. Ishu nzima ilichukua nafasi pande za Mbezi, Tanki Bovu kwa Mbona na sehemu nyingine kali, mimi na washikaji kibao tulikuwepo kwa ajili ya kutoa sapoti. Baada ya mpango huo, video imesafiri mpaka Ujerumani kwa ajili ya kufanyiwa 'editing', siku kadhaa zijazo itarudi Bongo tayari kwa kwenda hewani.

Read More......
Wednesday, March 30, 2011 Posted in | | 0 Comments »

Q Chiller na Meneja wake, Didas Facion

Kutoka pande za UK, Meneja wa msanii Abubakari Shabaan Katwila 'Q Chiller', Dida anayemiliki Kampuni yake ya mitindo, Didas Facion ameamua kuingia studio na kugonga ngoma yenye jina la Fake Niggaz ambayo itadondona Bongo mapema wiki hii kwa ajili na kwenda hewani kupitia vituo kadhaa vya redio kabla haijapigiwa kideo.

"Ngoma imetengenezwa na The Lodge Recording Studios In UK. Sasa nimeamua kukamata mic, nimechoka kuwadhamini wasanii kila siku wakati mimi mwenyewe game naliweza. Mimi ni mbunifu (facion) wa maisha, mwanajeshi wa kutafuta, popote naishi na chochote nafanya ili mradi kina kipato.

"Mimi ni mama wa watoto watatu na kwa wanangu ndiyo mama na ndiyo baba, sitegemei mwanaume, najitegemea na ujasiri wangu ndiyo uliyoniletea mafanikio katika maisha kwakuwa namuamini Mungu. Wengi wananifahamu kwa ujasiri wangu kama mwanamke mwanaume," alisema Dida kwa njia ya simu kutoka pande hizo.



Read More......
Posted in | | 0 Comments »

Linah (kulia) Chipukizi na Muimbaji bora wa kike
20% Aliibuka na tunzo 5
Hardmad naye aliambulia
Lamar mtayarishaji muziki bora

Inakuwaje Watanzania wenzangu na wapenda burudani? Mimi niko poa ile mbaya, naendelea kuwadondoshea ishu za ukweli kupitia hapa EBWANADAAH, blog yenu yenye kila aina ya za raha a.k.a burudani zinazoendelea kufanyika kila kukicha.

Mwishoni mwa wiki iliyopita macho na masikio ya Wabongo wengi vilikuwa pale ndani ya ukumbi wa Diamond Jubilee zilipofanyika sherehe za utoaji tunzo kwa wasanii wa muziki, watayarishaji video, muziki na wadau wengine wa sanaa hiyo waliyofanya vyema msimu uliyopita yaani 2010-2011.

Mimi pia nilikuwa ni miongoni mwa wadau wa burudani waliyokuwa makini kufuatilia kila 'kategori' ili kufahamu nani na nani watatunzwa baada ya kufanya vizuri mwaka jana ili nikufahamishe wewe mpenzi wa blog hii ambaye hukupata nafasi ya kuzicheki sherehe hizo kwa kuzama ukumbini au kupitia luninga yako a.k.a kitu cha live.

Najua wengine watakuwa wameshaanza kusahau kilichotokea siku hiyo na kuamua kuendelea na mishemishe za kusaka mkwanja huku wakibaki na viulizo kichwani kuhusiana na udhaifu uliyojitokeza siku hiyo. Lakini kwa kijana wa 'Farm Boyz' ya kule Kimanzichana, Habas Hamisi Kinzasa a.k.a 20% bado ni furaha kwa kwenda mbele na inawezekana asiisahau siku hiyo iliyompatia tunzo 5 za halali, zisizokuwa na skendo hata moja.

Ukweli ni kwamba, kila penye zuri, baya huwa linatafuta nafasi ya kujipenyeza na kutia dosari hata kidogo ili ishu nzima ionekana haikuwa poa. Binasfi nakiri kwamba, waandaaji wanastahili pongezi kubwa kwa kufanikisha kila kitu mpaka tunzo hizo kutua mikononi mwa wahusika, waswahili wanasema kuwa siku zote huwa hakuna shughuli ndogo hata kama ni arobaini ya kumtoa mtoto nje. Hivyo ninayo kila sababu ya kutoa 'rispekti' kwa Kilimanjaro na wote waliyofanikisha hilo, likiwemo Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA).

Lakini pamoja na pongezi hizo pia sitokuwa mnafiki kwa kuweka bayana yale machache yaliyozifanya sherehe hizo ziingie dosari. Kwakuwa mimi ni miongoni mwa wadau wa sanaa ya muziki nchini napenda tunzo hizo ziendelee kuwepo na kuwa bora zaidi kwani zinaleta changamoto kwa wasanii na tasnia nzima ya game hiyo Bongo kwani nikifunga domo langu sitohusika kwa namna moja ama nyingine katika kuziboresha, zaidi nafsi yangu itakuwa inanisuta.

Kama wewe msomaji haufahamu, yamekuwepo malalamiko kutoka baadhi ya wasanii wanaofanya maisha yao mikoani ambao majina yao yalitajwa kuwania tunzo hizo. Mmoja wa wasanii hao aliyepiga stori na Ebwanadaah ni Jetman anayeishi Harusha ambaye ngoma yake ilitajwa kuwania Tunzo ya wimbo Bora wa Ragga Dancehall, alisema kuwa alisikitishwa na kitendo cha waandaaji kutowajali wasanii wa mikoani waliyotajwa kuwania tunzo.

"Sijajua hizo tunzo zinaendeshwa kwa staili gani au zinawahusu wasanii wa Dar peke yao? Mimi nilishangaa kutoshirikishwa kwa chochote wakati wimbo wangu umeingizwa kwenye shindano. Wao kama waandaaji walitakiwa wawasiliane na mimi tangu kazi yangu ilipoingizwa, lakini mpaka zinakaribia fainali nilikuwa sijui chochote kinachoendelea, nikajaribu kupiga simu kwa wahusika ili nijue nitawezaje kushiriki katika sherehe hizo lakini wakawa hawapatikani na walipopatikana hawakupokea. Ninavyofahamu mimi msanii yoyote anayetajwa kuwania tunzo lazima awepo siku ya tukio ili kama atashinda akabidhiwe labda kama atakuwa na dharula ya muhimu, lakini Kibongo naona vinafanyika vitu kienyeji sana," alisema Jetman a.k.a Dizano anayefanya muziki wa 'dancehall'.

Ukweli ni kwamba, waandaaji wanatakiwa wawe wanajitahidi kuhakikisha kila msanii ambaye kazi yake imetajwa kuwania tunzo hizo anakuwepo ili kuepuka ile hali ya nani akamchukulie fulani kama ilivyotokea kwenye kategori ya Msanii Bora wa kike ambapo Lady Jaydee alichukuliwa tunzo yake na shabiki baada ya kimya cha muda na watu kusubiri huenda Jide ataibukia kona fulani ya ukumbi lakini wapi, wala haikuelezwa sababu za yeye kutokuwepo kama ilivyokuwa mwaka jana ambapo mumewe Gadner alipomtetea kwamba ameshindwa kuhudhuria kwenye tunzo hizo kwasababu alikuwa na kazi katika ukumbi mmoja wa burudani, hivyo aliheshimu mkataba wake.

Vivyo hivyo katika Wimbo Bora wa Afrika Mashariki, kama tumeamua kwenda Kiafrika Mashariki basi siyo mbaya wasanii hao wakipewa mualiko ili kama wanashinda wakabidhiwe tunzo zao, lakini siku hiyo Kidumu kutoka Kenya sikumuona na haikutajwa sababu yoyote ya yeye kutokuwepo zaidi ya kuchukuliwa tunzo yake na shabiki. Mbona sisi huwa tunazifuata zile za Kisima kule Kenya, Parm (Uganda), MTV Afrika, Channel O, Kora na nyingine ambazo huwa zinatuhusu. Amini nawaambia kwa kufanya hivyo heshima kubwa itashuka kunako tunzo hizo. Kingine ni kwamba ile shoo kali mliyotuahidi kutoka kwa wasanii wetu wa nyumbani ambao mliwalipa vizuri mbona sikuiona? Nilichokiona mimi ni kile nilichokizoea siku zote ambacho sikuhitaji kukitia machoni tena, kwani wasanii ni wale wale na nyimbo ni zile zile.

Mimi kama mdau wa burudani nauliza kwamba; Hivi Tanzania haina wasanii wapya wanaofanya vizuri ambao watu wanahitaji kuwaona jukwaani, kama hawapo mbona kwenye kategori zenu zipo za wasanii chipukizi? Kama mlikuwa hamjui Wabongo wengi nikiwemo mimi tunahitaji vitu vipya kila siku na siyo shoo zile tulizozoea za mtu mmoja kusimama jukwaani na kupiga kelele kisha anashuka, anatia mkwanja wake mfukoni anasepa. Nilitegemea kuona wasanii kama Linex, Sam wa Ukweli, Ben Paul, Beka, Ditto, Mataluma, Dogo Janja, Godzilla, Belle 9 na wengine wengi wanaofanya vyema hivi sasa wanapata nafasi ya 'kupafomu' stejini.

Pia zamani sheree hizo zilikuwa zinapambwa na ngoma za asili kutoka katika vikundi mbalimbali akiwemo Wanne Star, lakini siku hizi ni muziki wa kizazi unachukua nafasi kubwa, ambao kwa jinsi wasanii wetu wanavyofanya unaonekana hauna mvuto jukwaani. Kama hamuamini hilo mnakumbuka mashabiki walivyowapokea kina Banana walipoimba wimbo wa Msondo, Binadamu tumeumbwa mateso? Msifikiri wote wanaokuja pale wanapenda Hip Hop. Yapo matatizo mengine mengi ambayo kama hayatorekebishwa yatazifanya tunzo hizo zizidi kupoteza mwelekeo kila mwaka, inawezekana siyo makosa ya waandaaji bali ni ya wale wanaojiita wadau ambao wanapopata nafasi ya kushiriki kufanikisha shughuli hiyo huitumia vibaya, pengine kwa kutokwa na uelewa kuhusu sanaa ya muziki au kujisahau. Ni hayo tu.

Wenu katika kuboresha tunzo hizo.

MC George.

0715 110 173


Read More......
Posted in | | 0 Comments »

Marehemu Issa Kijoti, enzi ya uhai wake
Baadhi ya wanamuziki wa kundi la 5 Star Morden Taarabu waliyofariki dunia kwa ajali ya gari iliyotokea pande za Mikumi, Morogoro usiku wa kuamkia jana, wameanza kuzikwa baada ya taratibu zote za mazishi kukamilika.
Kwa mujibu wa watu wa karibu na familia zao, Marehemu Issa Kijoti alizikwa jana usiku mara baada ya mwili kuwasili nyumbani kwao Mtoni kwa Aiziz Ally, Dar majira ya jioni. "Wapo waliyosafirishwa kwenda kuzikwa makwao ukiachilia mbali wale waliozikwa Dar," .
Msiba huo wa zaidi ya wasanii 12 waliyofariki katika ajali hiyo umeacha simanzi kubwa kwa wapenzi wengi wa muziki huo na jamii nyingi kwa ujumla. Mungu Aziweke Roho zao Mahali pema Peponi, Amen.

Read More......
Wednesday, March 23, 2011 Posted in | | 0 Comments »

UNAJUA BADUGU NI NINI? KAA TAYARI

Read More......
Monday, March 21, 2011 Posted in | | 0 Comments »

Hapa tukimshangaa samaki wa ajabu tuliyemkuta mchangani
Unamuona vizuri

Kisha nikaendelea na mazoezi

Juzi kati, yaani Machi 19, ilikuwa ni siku yangu ya kuzaliwa. Kwanza namshukuru Mungu kwa kuniongezea mwaka mwingine tena kwani wapo waliyotamani kuifikia siku hiyo lakini haikuwezekana. Pia nawashukuru wote waliyonikumbuka na kunitakia Birthday njema, Mungu awabariki sana. Siku hiyo jioni niliamua kwenda kujipumzisha na kufanya mazoezi ufukweni mwa bahari pande za Kawe. Wakati naendelea na mazoezi mchangani nikakutana na kiumbe cha ajabu, ni samaki ambaye aliwashangaza wengi waliyokuwa maeneo hayo (kama anavyoonekana pichani). Wewe mdau wa ebwanadaah unajua jina la samaki huyo. Siyo mbaya ukinijuza, siunajua mimi mtu wa bara.

Read More......
Posted in | | 0 Comments »


Kutoka Block 41, KInondoni, Dar ilipo kambi ya 'Kikosi cha Mizinga', kiongozi wa umoja huo, Kalama Masoud 'Kalapina' yuko tayari kwa utambulisho wa albamu yake mpya, 'Nyimbo Tosha' utakaochukua nafasi ndani ya Club Maisha, Machi 26 mwaka huu. "Natarajia kupewa sapoti na wasanii kama Madee, A.Y, FA, THT na wengine kibao wakiwemo Ukoo flani kutoka Kenya na Black T kutoka Rwanda," alisema na ebwanadaah.

Read More......
Posted in | | 0 Comments »

Andru G na Skora katika pozi

Kupitia ndani ya video mpya ya ngoma ya Skora ya kwake, Adru G utakutana na sura ya mrembo mmoja wa kijanja ambaye ameakti kama Skora na kuonesha uhalisia wa kutosha. Video hiyo ambayo itadondoka hewani muda wowote kuazia sasa inatarajia kumrudisha Andru kwenye game kama zamani alipofanikiwa kufanya 'wonder' na nyimbo kadhaa.

Read More......
Posted in | | 0 Comments »

Kutoka 24/7 Records Mikocheni, Dar huyu hapa Mahamud Issa a.k.a Wyname ambaye hivi sasa amekuja vizuri na ngoma yenye jina la Japo Kidogo akiwa amempa shavu swahiba wake Sunday Mangu a.k.a Linex (Linenga). Kama hujamsoma vizuri ndiyo mchizi aliyegonga korasi ya ngoma ya SMS ya kwake Nick Maujanja na nyingine kibao. Hivi karibuni mchizi alikuwa ni miongoni mwa wasanii kumi nikiwemo mimi waliyofanya ngoma yenye jina la Tusaidie iliyofanyika ndani ya studio hizo kwa ajili ya kuwafariji waathirika wa mabomu Gongolamboto. Isikilize ngoma ya Wyname, Japo kidogo hapo juu kushoto.

Read More......
Posted in | | 0 Comments »






Huyu ndiye Skyner, binti aliyefanya vizuri ndani ya muvi mpya ya Ray yenye jina la The Second Wife. Mrembo huyu amefunguka ndani ya Ebwanadaah kwamba ameingia kwenye sanaa hiyo kikazi zaidi na siyo mapenzi. "Unajua wabongo wakikuona kwenye filamu tu, wanajua tayari, kwangu mimi no," alisema Skyner.

Read More......
Tuesday, March 8, 2011 Posted in | | 4 Comments »





UNAWEZA usiamini, lakini ukweli ni kwamba Meneja wa kundi la TMK Wanaume Family, Said Hassan Fella amegeukia upande mwingine wa sanaa ya muziki, safari hii akigonga muziki wa mwambao a.k.a taarabu na tayari ameshajitambulisha kwa kazi moja aliyompa shavu Isha Ramadhani a.k.a Mashauzi kutoka ndani ya Kundi la Jahazi.
“Kazi inaitwa…….. imefanyika ndani ya studio za Kubwa Records zilizopo Temeke Mikoroshini. Unajua muziki hauna mipaka ndiyo sabab iliyonifanya niibukie kwenye muziki wa taarabu, najua wengi watashangaa lakini kiukweli wasanii wa Bongo tunatakiwa tubadilike badala ya kung’ang’ania sehemu moja miaka yote,”-Fella.
Fella alisema kuwa kwasasa ametoa ngoma hiyo moja ili kuwauliza mashabiki wa pande hizo kuwa aendelee au asiendelee, kisha atachukua maamuzi kutokana na wadau watakavyompokea upande huo wenye fans wengi wa kike.

Read More......
Posted in | | 0 Comments »



KIMWANA aliyewahi kuiwakilisha Tanzania kwenye shindano la visura, Nokia Face Of Afrika 2006 na mwanamuziki wa kizazi kipya, Zuhura Mrisho alicheki na sisi kwa njia ya simu kutoka Kanda ya Ziwa na kutamka kuwa hivi karibuni alijikuta ametaitiwa na wanafunzi wa shule moja mkoani Mwanza wakitaka wagongewe ‘free style’.
“Yaani ilikuwa balaa, nilikuwa katikasha stendi kuu ya mabasi hapa Mwanza, ghafla wakatokea wanafunzi wengi wakanizunguka na kunambia, “bibi babu yuko wapi, tunataka mtuimbie kidogo wimbo wa Hadithi, ikabidi nimpigie simu George MC aliyekuwa Dar ambaye nilifanya naye wimbo huo akaongea na watoto hao, waliporidhika wakaniachia huku wakihitaji siku moja watuone live tukiimba,”- Zuhura.

Read More......
Posted in | | 0 Comments »

Godfrey Tumaini ndiyo jina lake na Dudubaya ndiyo jina la kazi lililokataa kufutika kwenda kwenye Duduzuri. Mchizi amesema na sisi kwamba siku hizi haonekani Dar es Salaam ‘Town’ kwakua hakuna ishu.

“Unajua watu wengi watakuwa wanajiuliza Dudu siku hizi yuko wapi? Ukweli ni kwamba ‘Town’ siku hizi hakuna ishu ndiyo maana mimi sitokei pande hizo, mara nyngi nakuwa mikoani kwenye shoo ambako ndiko biashara ya muziki ilikobaki. Kwa mfano hivi sasa nina shoo zaidi ya tano Kanda ya Ziwa, huwa natokea Dar siku moja moja kasha napotea,”- Dudu.

Read More......
Posted in | | 0 Comments »