ILI MUZIKI WETU UWEZE KWENDA KIMATAIFA NI LAZIMA TUBADILIKE, SAPOTI YAKO PIA MUHIMU

“Habari yako bana….hop unaendelea poa na kazi, ni hivi ndugu yangu, niliwahi kuambiwa msemo

fulani, kuwa katika kila utakalofanya au litakalotokea basi lazima watu wataongea, kwamba ulichofanya sio sahihi. Ikiwa ina maana kuwa watu mara zote hawaridhiki na kile kinachotokeaga.

Kwanini nimetoa mfano huu? kwa sababu hiyo niliyosema hapo juu kwamba watu lazima wataongea tu!! kwa kila kitakachotokea, LAKINI SIO MARA ZOTE WANAONGEA KIMAKOSA TUU, wakati mwingine matatizo yanaonekana wazi, kwahiyo lazima yaongelewe….BACK IN BUSINESS….. TUZO/TUNZO za kili, naamini TUZO ndio sahihi …nway, zimetolewa juzi kati na waliopata wamepata…aya nawapa hongera zao, maana wametengeneza historia ya maisha ya mziki wao, lakini je kweli wanastahili kupata tuzo hizo? wanastahili kuwepo kama nominees katika hizo categories? Wanafanya aina hiyo ya mziki ambao wameshindia hiyo tuzo? haya ni maswali ya kujiuliza, siwafahamu waliopo kwenye kamati husika ya tuzo hizi, ila naamini watakuwa na uelewa wa mziki wetu, lakini kwa hili la kutokea kila mwaka linanipa mashaka.

Hivi tunawezaje kusema basketball imepiga hatua ikiwa kila ligi, kila mwaka timu zinazoingia fainali ni SAVIO na VIJANA? kikapu kitakuwa hakijakua maana vipawa vipya havionekani? au nyie mnatazama katika nyanja zipi? kama sio hizi za baada ya kazi ngumu lazima utunukiwe tuzo. Jee kweli havionekani? Na kipi kinasababisha visionekane? na je hilo sio jukumu la hawa waandaaaji wa tuzo hizo? Obviously itakuwa ni jukumu lao, maana kati ya hao waandaaji naamini wapo maproducers, nadhani hata mapresenters na d.j’s wa radio na t.v pia na wadau kwa ujumla wa mziki huu pia…..!! 2009-2010 binafsi naamini kabisa game ya mziki wetu ilibadilika sana, na kutawaliwa na chipukizi, ambao wengi wamefanya vizuri sana kuliko hawa wasanii wengine ambao wapo kwenye game kwa muda mrefu. Izzo b, nikki wa pili, roma, Quick r…., diamond, belle9, lina, barnaba, pipi, amini, na wengineo wengi, siwezi kuwataja wote na haina maana kuwa kama sijakutaja hapa ndo’ hufai…. lah hasha!! hayo ni baadhi ya majina yaliyonijia haraka tu, hawa mbona walifanya vizuri na waliweza kusimama bora zaidi…je tunawaingiza kwenye category moja tu ya msanii anaechipukia? hapana…mbona ktk category ya msanii bora wa RnB yupo steve, Belle 9, diamond, A.T, hawa wengi wao ni chipukizi kama sio wote…which means waliweza kufanya vizuri zaidi ya wale waliotangulia kwenye game hii, si ndio? aya tuangalie na upande mwingine wa shilingi, je tukirudi kwa upande wa wanaofanya mziki wa RAP… ina maana hawa hawakupata upinzani kutoka kwa upcomingz artists wengineo zaidi ya Quick r….. tu?mbona kila mwaka ni kama nominees ni walewale tu wanajirudia?mziki (rap game)tuseme haikui?wao ndo’ bora kila mwaka kweli? ha ha ha ha ha!! ni Quick r…peke yake ndo aliweza kucompete na hawa watu tu? what about roma? Na je nikki wa 2? Business nae pia? hata kala jeremiah pia? Au ni vigezo gani vinatazamwa katika hili? Na hao nominees wote au wengi wao wame base kwenye topic moja tu, kujisifu wao ndio wanai-run hii game kuliko wengine, huyu anajiita professional , yule anasema anatuvua kama samaki, huyu nae anatuambia tumpishe, huku anatupigia honi…. pom pom pom pishaaaa. IZ DAT HIP HOP????mtu anasema NINA PESA MINGI MPAKA NATAMANI JITEKA…THEN WATU WAPO KING STONE KAMA JAMAICA….thats hip hop????? vipi kuhusu huyu aliyesema…. MIGOMO YA CHUO KIKUU NAITUPIA JICHO LA TATU…SITETEI MPAKA RUTASHOBORWA AKIWA WAKILI KISUTU…kwa tafsiri ya haraka haraka nani anafanya hip hop real kati ya hawa? nani anaongea real? ni kweli ana pesa nyingi kiasi hicho hadi anatamani kujiteka?Nway HIP HOP ina vitu vingi ikiwemo consciousness na free styl pia, pengine yoyote atakayechagua moja wapo kati ya hivyo vitu viwili atakuwa ameitendea haki, so may be wana diserve. Msiseme kuwa siku zote nilikuwa wapi sikuongea, maana maneno hayaozi na ukweli utaendelea kuwepo tu. Sitaki kuliongelea hili la HIP HOP, lakini nitaligusia, wengi wanaamini mziki wa HIP HOP ni ule unaozungumzia REALITY,(maisha halisi),kutetea haki, kutoa elimu, kukosoa nakadhalika, but i-base katika sense na consciousness, lakini tunaona nominees wa categories kama hizo hawahusiani na huo uhalisia wa HIP HOP, mfano halisi kwenye nyimbo zao hizo zilizoshiriki? au HIP HOP ni kuwa na beat ngumu tu? ha ha ha ha ha!! nway hata wenzetu wa America tunaona katika hili pengine wanasuasua ndomana nasi pia, kwa maana vingi tunavitoa kwao.

Mashabiki ambao ndo ‘ wanapiga kura, wengi wao hawafuatilii mziki kwa undani na umakini zaidi, mimi naamini hilo, mfano nitakupa……..” watakapoona kwenye category ya muandishi bora wa nyimbo ya RAP yupo ROMA na ngoma yake ya MR.RESIDENT na yupo na flani na wimbo wake ambao kimsingi huyo flani amesifia tu pombe na starehe za club, hata kama huo wimbo hauna maana, lakini kwa vile tu huyo msanii flani ana album, ni mkongwe, anajulikana sana na alitamba na ngoma nyingi sana basi utakuta shabiki ana vote kwa huyo msanii flani, pasipo kujua tuzo inataka nini katika hiyo category…tena utamkuta anasema aaaah!! ROMA mtoto wa juzi tu atamuweza huyu flani, huyu mkongwe sana, huyu flani alihit na ngoma yake ile ya………….apo anakumbushia ngoma ya nighteen kweusiiiii….wakati award haitaki nyimbo hiyo… hicho ndicho mashabiki wengi wanakifanya….Hivi tujadiliane hili unaposema watu watume sms kumchagua msanii bora wa kitu flan, halafu yule artist akawapanga watu wake wampigie kura na wakampigia kura akashinda, je hapo tutakuwa tumemchagua yeye kama bora au? ok sio asilimia zote za kura hutoka kwa wananchi, je nyie majaji mnaangalia vigezo gani? nafahamu kwenye mkutano wenu kabla ya kuanza kuvote mlitaja vigezo vyenu, lakini bado nina shaka na hilo.

Ili msanii afanye vizuri anatakiwa awe na presentation nzuri, production safi na promotion pia iwe ya nguvu zaidi, lakini kwetu hapa bongo hutokea mara chache sana hivyo vitu kuwa kama vigezo vya kufanya vizuri, itz like hakuna formula inayomfanya mtu akafanya vizuri hapa kwetu, tunaona wasanii wanatoa nyimbo za ajabu ajabu lakini zinaheat, sasa nauliza huo ubora wanaoutazama killi award je ni kwa ajili ya air tym hiyo wanayopata hao wasanii au?kama ndivyo je yule atakayeweza kujifanyia air time ya nguvu kubwa ndio ataibuka mshindi? Pengine mimi sijajua ubora wa nyimbo ni upi? labda ni midundo iwe mikali na vocal ziwe safi na sound iwe poa halafu humo katikati utupie mashairi yako ya mitindo huru yasiyokuwa na maana katika kiwango cha kutosha…… Sitaki na sipendi mtu anaposema mbona America wanafanya hivi…kwani si wao!!ok sisi tunacopy kwao lakini isiwe kila kitu jamani, tukishindwa kabisa sawa tuvicopy, lakini tutazame na sehemu ya kuvipaste pia jamani. Wimbo bora wa mwaka, je ni bora kuanzia tungo, midundo, upangiliaji wa mashairi,sauti,style na vingine muhimu? au ni bora kwa sababu unajulikana sana na watu wanaiimba hadi watoto!! je huo ndo ubora? na yule ambae hajajulikana wala kusikika sana je yeye siyo bora? Basi ni vema hata majina ya categories yakabadilishwa pia. Labda tuite wimbo uliopigwa sana na vituo vya radio, au club, msiniambie kama kilichobora ndo’ hupigwa, eti kama sio bora kisingepigwa…aaaah waaapi….!!mapepe ya kingwendu au kamongo ya mr.ebbo zilipigwa sana kipindi hicho,….pengine zilikuwa bora, mimi sina comments hapo.

Nafahamu wengi wakipata tuzo hakuna hata mmoja atakayeweza kusema hazipo fair kwa sababu amepata, lakini angekosa najua angefunguka tu, yaani huwezi kumfuata mwalimu wako na kumwambia mwalimu umenipatisha….aaaah waaapi!!! hata siku moja. So sisi ndio tuna nafasi kubwa ya kuliona hilo.

Nafurahi kuona vitengo na wadau mbalimbali wanajitokeza kuanzisha tuzo zao, kwa ushauri tu ni vema zikaboreshwa zaidi ya hizi zilizopo sasa, ili mabadiliko chanya yaweze kuonekana…

Kwa ushauri wangu mchanga ningeweza kuwa – advice wanakamati wajipange kuwa na tuzo nyingi na waongeze categories pia…

Kila mtu ana uhuru wa kuongea na kocomment kutokana na hizi tuzo,japo kuwa sio lazima….ila ROMA amezaliwa kukosoa vilivyopinda.

Waliopata tuzo al hamdllh….waliokosa next tym famil-lah ol of ‘em BIG UPS!!!!maisha yanaendelea na mziki unaendelea.....ila ukweli siku zote una tabia ya kushinda…no matter how long will take…..CONSCIOUS FOREVER………….O…N…E”

Read More......
Tuesday, May 18, 2010 Posted in | | 0 Comments »

Party people!

Tickets to the Full Moon party are now on sale! For the first time ever in Kampala, Talent 256 brings you the best music and lighting, visuals, and many more surprises - all under the moon and stars!

We’ll have a bus running from central Kampala, and plenty of secure parking at the venue if you prefer to drive. Cash bar and lots of snacks will be available all night, so bring your dancing shoes and prepare for an unforgettable party!

It all goes down on Friday, May 28th at Kamooflage Paintball Munyonyo, next to Speke Resort. Get your tickets now for 25,000 or pay 30,000 at the door.

Call the ticket hotline at 0782 506 684 to get yours!

Read More......
Posted in | | 0 Comments »





Mkali wa dancehall kutoka pande za Marekani, Sean Kingston jana usiku alimaliza kibarua kilichomleta Bongo kwa kuangusha burudani ya ukweli pale Diamond Jubilee. Kama haukuwepo pande zile utakuwa umekosa burudani nzuri iliyowarusha mashabiki kibao. Lakini siyo mbaya, huenda siku nyingine akaalikwa tena Bongo.

Read More......
Sunday, May 16, 2010 Posted in | | 0 Comments »

Baba na mwana
Marlaw
Johmakini
Chid Benz
A.Y
AT
Bwana Misosi
Chokoraa
Lamar
Mzee Yusuf
Diamond
Mimi pia nilikuwepo, hapa nikiwa na mdau John (kushoto)
Hapa niki-shoo love na Prof. J (kulia)

Mchakato mzima ulifanyika ndani ya Ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar Ijumaa, May 14, 2010. Wacheki washindi wote hapo chini.

Mwimbaji Bora wa Kike

Lady Jaydee

Mwimbaji Bora wa Kiume

Banana Zorro

Albamu Bora ya Taarab

Jahazi Modern Taarab (Daktari wa Mapenzi)

Wimbo Bora wa Taarab

Jahazi Modern Taarab (Daktari wa Mapenzi)

Wimbo Bora wa Kiswahili (Bendi)

African Stars Band (Mwana Dar es Salaam)

Albamu Bora ya Bendi

African Stars Band (Mwana Dar es Salaam)

Wimbo Bora wa R&B

Diamond (Kamwambie)

Wimbo Bora wa Asili ya Kitanzania

Mrisho Mpoto (Nikipata Nauli)

Wimbo Bora wa Hip Hop

Johmakini (Stimu Zimelipiwa)

Wimbo Bora wa Reggae

A.Y- (Leo, Reggae Mix)

Wimbo Bora wa Ragga

Bwana Misosi (Mungu Yupo Busy)

Rapa Bora wa Mwaka (Bendi)

Chokoraa

Msanii Bora wa Hip Hop

Chid Benz

Wimbo Bora wa Afrika Mashariki

Kidumu ft. Juliana (Haturudi Nyuma)

Mtunzi Bora wa Nyimbo

Mzee Yusuf

Mtayarishaji Bora wa Nyimbo

Lamar

Video Bora ya Muziki ya Mwaka

CPWAA (Problem)

Wimbo Bora wa Afro Pop

Marlaw (Pipii-Missing My Baby)

Msanii Bora Anayechipukia

Diamond

Wimbo Bora wa Kushirikiana

AT ft. Stara Thomas (Nipigie)

Wimbo Bora wa Mwaka

Diamond (Kamwambie).

Read More......
Posted in | | 0 Comments »




Jana nilifanya ziara ndani ya studio za 24 zilizopo pande za Mikocheni, Dar na kukutana na prodyuza mkali, Villy na kupiga naye stori mbili tatu ikiwa ni kubadilishana mawazo kuhusu game ya muziki wetu wa Bongo ulipotoka na unapokwenda sasa. Baada ya stori kadhaa nilisikiliza baadhi ya kazi alizofanya nikagundua kwamba jamaa ni mkali ile mbaya, ni miongoni mwa maprodyuza wachache hapa TZ ambaye wanaweza kuleta mapinduzi makubwa na kuufikisha muziki wetu mbali kama wadau watamtumia vizuri. Kama hauamini hebu mcheki pande hizo ili ujionee kazi zaidi.

Read More......
Friday, May 14, 2010 Posted in | | 0 Comments »


Siku kadhaa zilizopita mwenyezi Mungu alinikutanisha na msanii huyu mwenye a.k.a ya Diblo ambaye ana uwezo mkubwa wa kucharaza gita na kuimba. Kiukweli sikuamini baada ya kusikiliza baadhi ya kazi zake, nikagunfdua kumbe kitaa kuna vioaji vingi ambavyo bado watu hawajaamua kuviopa sapoti ili jamii iweze kuvisikia na kujifun za kutoka kwao. Kilichofuata baada ya hapo nimejitolea kumsaidia kwa kadri ntakavyoweza ili jamii ipate kumfahamu. Vipi wewe mdau wa burudani, unaweza kuungana nami katika kusaidia kuendeleza kipaji cha Diblo kwa kunicheki kupitia 0715 110 173 au email iliyopo hapo juu..

Read More......
Posted in | | 0 Comments »



Kama wewe ni shabiki wa bluu, basi ungana nami katika ushindi huu wa kutosha, bao 8 siyo mchezo. Man yeye kaambulia 4-0 ameshika nafasi ya pili.

Read More......
Sunday, May 9, 2010 Posted in | | 0 Comments »

Mfalme wa Rhymes, the one no succeeded, Suleiman Msindi ‘Afande Sele’, wiki iliyopita ‘aliisapraiz’ blog hii baada ya kuidondoshea SMS kali kuhusu Bongo Fleva. Unaweza kuisoma hapo chini;

“Miti mirefu na mikubwa inapoangushwa huangukia ile midogo na mifupi. Hivyo pamoja na waangamizaji kufanikiwa kuangusha na kuangamiza miti mirefu na mikubwa kama ilivyokuwa na inavyoendelea wakati huu, bila shaka na miti midogo yote itaendelea kuangamia tena kwa wingi zaidi kuliko ile mikubwa michache inayokatwa kila siku.

“Kwa mtindo huu basi siku miti mikubwa itakapokatwa na kuangushwa yote ikamalizika msituni, ndiyo wakati pia hakutakuwa wala kuonekana hata mti mdogo utakaosalia msituni ukiwa umesimama wima, kwani muanguko wa miti mirefu na mikubwa ambayo bila shaka itakuwa ni mizito pia itakuwa imeangamiza miti midogo yote msituni na kuiponda kabisa kama baadhi ya Ma-Dj wa redio wataendelea kubania wakongwe kwa nia ya kuwaua kimuziki basi wataua na wadogo.

“Hivi sasa kila mtu anajidai anaijua Bongo Fleva kuliko hata wajuzi na wazoefu wa game hili, Bongo Flava inakua upande wa uimbaji lakini marapa wapya hakuna anayeishika jamii. Wengi wana mashairi dhaifu sana na idea ni za kitoto.

“Wengi wanabebwa na ma-Dj wenye maslahi nao. Kuna Ma-Dj wanawaumiza makusudi wakongwe hata kazi zao za ukweli wanazibana wakidhani wanaua wakongwe kumbe wanaliua game zima. Wanakata nguzo kuu ambazo ni mashairi na ujumbe bora toka kwa wakongwe ambao wanatambua haki zao.

“Walionyonywa ni wengi, wanaharakati wa ukweli! Sasa jamii inapaswa kuamka na kudai kile cha ukweli na si kuamini kila wanachokisema ma-Dj walioanza kazi juzi wakati game imetolewa mbali tena kwa machozi, jasho na damu.

“Watu wanapaswa kujua kwamba Watanzania ni walewale na si wajinga kama baadhi ya Ma-Dj na watangazaji wanavyofikiri kuwa kila wanachotaka wao basi Wabongo wataamini. Leo hii kuna artists wanapewa promo kila siku kwa kulazimisha lakini bado ukija huku mtaani watu bado hawawajui kwakuwa mchango wao katika game haufanani na sifa wanzopewa.

“Shabiki wa Afande, Prof. Jay, Daz Nundaz ndiyo huyo huyo atakayemkubali na artist mpya anayetoka vyema katika game, sasa kama kutoka kwa wasanii wapya dhaifu ndiyo kunasababisha kuwaua wakongwe wa ukweli, basi mashabiki hawatoendelea kuamini game na matokeo yake hadhi ya muziki inashuka.

“Katika jamii, kitendo cha watangazaji fulani na ma-Dj kutowapa nafasi waasisi, basi na jamii haitokubali au kumtambua msanii mchanga anayekuzwa kwa uongo na ufisadi unaofanywa na ma-Dj pamoja na mameneja uchwara wanaoshinda wakihonga na kuleta fitina ya wasanii na watangazaji, lakini ukweli unatashinda.”

Read More......
Friday, May 7, 2010 Posted in | | 0 Comments »

Kalapina

Mansul

Shoo ya mkali wa steji ambayo ipo organized by Kikosi cha Mizinga, iliyotibuliwa na mvua na kutofanyika kama ilivyotangazwa awali, itachukua nafasi Jumapili ya wiki hii pale pembezoni mwa fukwe za Coco zilizopo Oysterbay, Dar.

President wa Kikosi, Karama Masoud ‘Kalapina’ alisema: “Ngoma itafanyika Jumapili hii, eneo la tukio ni lile lile, Coco Beach na watu waje ili kumjua nani mkali wa kumiliki jukwaa kati ya Mansul, TMK Halisi, Rado, Bon Crew na wengine kibao.”

Read More......
Posted in | | 0 Comments »


A.Y
FA

R.O.M.A
Mike Tee

Wanasema Bongo Fleva hailipi. Wanadai imepotea njia lakini guys wanaendelea kusimamisha topic ambazo zinawapa ushujaa kitaani ikiwemo kuendelea kuipa heshima game hiyo. R.O.M.A, A.Y, FA, Tip Top Connection na Mike Tee wamedondosha ngoma mpya kitaa wiki mbili zilizopita ambazo zimesimama inavyotakiwa. R.O.M.A amedondoka na kitu Pasta Watatu, Tip Top wapo na ngoma Bado Tunapanda, Mike Tee yeye anayo Tujiibe tukiweza wakati FA na A.Y wamesimama pamoja katika dude linalopatikana kwa jina la Usije Mjini.



Read More......
Posted in | | 0 Comments »

Mratibu wa mpambano huo katika pozi







Kinyang'anyiro cha kumsaka mrembo wa Kilimanjaro 2010 kiko njia moja, zaidi wa warembo tisa (pichani) wanatarajiwa kupanda stejini Juni 11, mwaka huu kwa ajili ya kumtafuta mshindi atakayeuwakilisha mkoa huo kwenye fainali za Miss Tanzania. Ili kujua wapi na lini mpambano huu utafanyika endelea kufuatilia blog hii ya kijanja.

Read More......
Sunday, May 2, 2010 Posted in | | 0 Comments »


"Noma kweli, baba yangu amefariki, msiba uko Kinyerezi, Dar. Kwa yeyote atakayependa kuja, anashuka gereji, pembeni kuna duka la mbao akifika hapo anauliza kwa Zay B. Tunasafirisha leo kwenda Iringa kwa mazishi, kesho Jumatatu tutarudi kwasababu msiba utaendelea kuwa Kinyerezi," alisema Zay B kupitia ujumbe mfupi wa maandishi.

Read More......
Posted in | | 0 Comments »