ILI MUZIKI WETU UWEZE KWENDA KIMATAIFA NI LAZIMA TUBADILIKE, SAPOTI YAKO PIA MUHIMU

Mfalme wa Rhymes, the one no succeeded, Suleiman Msindi ‘Afande Sele’, wiki iliyopita ‘aliisapraiz’ blog hii baada ya kuidondoshea SMS kali kuhusu Bongo Fleva. Unaweza kuisoma hapo chini;

“Miti mirefu na mikubwa inapoangushwa huangukia ile midogo na mifupi. Hivyo pamoja na waangamizaji kufanikiwa kuangusha na kuangamiza miti mirefu na mikubwa kama ilivyokuwa na inavyoendelea wakati huu, bila shaka na miti midogo yote itaendelea kuangamia tena kwa wingi zaidi kuliko ile mikubwa michache inayokatwa kila siku.

“Kwa mtindo huu basi siku miti mikubwa itakapokatwa na kuangushwa yote ikamalizika msituni, ndiyo wakati pia hakutakuwa wala kuonekana hata mti mdogo utakaosalia msituni ukiwa umesimama wima, kwani muanguko wa miti mirefu na mikubwa ambayo bila shaka itakuwa ni mizito pia itakuwa imeangamiza miti midogo yote msituni na kuiponda kabisa kama baadhi ya Ma-Dj wa redio wataendelea kubania wakongwe kwa nia ya kuwaua kimuziki basi wataua na wadogo.

“Hivi sasa kila mtu anajidai anaijua Bongo Fleva kuliko hata wajuzi na wazoefu wa game hili, Bongo Flava inakua upande wa uimbaji lakini marapa wapya hakuna anayeishika jamii. Wengi wana mashairi dhaifu sana na idea ni za kitoto.

“Wengi wanabebwa na ma-Dj wenye maslahi nao. Kuna Ma-Dj wanawaumiza makusudi wakongwe hata kazi zao za ukweli wanazibana wakidhani wanaua wakongwe kumbe wanaliua game zima. Wanakata nguzo kuu ambazo ni mashairi na ujumbe bora toka kwa wakongwe ambao wanatambua haki zao.

“Walionyonywa ni wengi, wanaharakati wa ukweli! Sasa jamii inapaswa kuamka na kudai kile cha ukweli na si kuamini kila wanachokisema ma-Dj walioanza kazi juzi wakati game imetolewa mbali tena kwa machozi, jasho na damu.

“Watu wanapaswa kujua kwamba Watanzania ni walewale na si wajinga kama baadhi ya Ma-Dj na watangazaji wanavyofikiri kuwa kila wanachotaka wao basi Wabongo wataamini. Leo hii kuna artists wanapewa promo kila siku kwa kulazimisha lakini bado ukija huku mtaani watu bado hawawajui kwakuwa mchango wao katika game haufanani na sifa wanzopewa.

“Shabiki wa Afande, Prof. Jay, Daz Nundaz ndiyo huyo huyo atakayemkubali na artist mpya anayetoka vyema katika game, sasa kama kutoka kwa wasanii wapya dhaifu ndiyo kunasababisha kuwaua wakongwe wa ukweli, basi mashabiki hawatoendelea kuamini game na matokeo yake hadhi ya muziki inashuka.

“Katika jamii, kitendo cha watangazaji fulani na ma-Dj kutowapa nafasi waasisi, basi na jamii haitokubali au kumtambua msanii mchanga anayekuzwa kwa uongo na ufisadi unaofanywa na ma-Dj pamoja na mameneja uchwara wanaoshinda wakihonga na kuleta fitina ya wasanii na watangazaji, lakini ukweli unatashinda.”

Friday, May 7, 2010 Posted in | | 0 Comments »

One Responses to "NEW SMS KUTOKA KWA AFANDE SELE"

Write a comment