Jana nilifanya ziara ndani ya studio za 24 zilizopo pande za Mikocheni, Dar na kukutana na prodyuza mkali, Villy na kupiga naye stori mbili tatu ikiwa ni kubadilishana mawazo kuhusu game ya muziki wetu wa Bongo ulipotoka na unapokwenda sasa. Baada ya stori kadhaa nilisikiliza baadhi ya kazi alizofanya nikagundua kwamba jamaa ni mkali ile mbaya, ni miongoni mwa maprodyuza wachache hapa TZ ambaye wanaweza kuleta mapinduzi makubwa na kuufikisha muziki wetu mbali kama wadau watamtumia vizuri. Kama hauamini hebu mcheki pande hizo ili ujionee kazi zaidi.
Friday, May 14, 2010
Posted in | |
0 Comments »
One Responses to "NDANI YA 24/7 RECORDS NA VILLY"