Niaje wadau, mkoa poa? Kwanza kabisa nachukua nafasi hii kuwaomba radhi kwa kuwa kimya kwa muda, ila waswahili husema, Kimya kingi kina mshindo mkuu, nilikuwa tait kunako mishemishe za kumalizia video ya ngoma yangu 'NARUDI NYUMBANI' niliyowashirikisha Zuhura na Cheleaman ambaye kwasababu zilizokuwa nje ya uwezo wake hakuweza kuonekana kwenye video hii (kama mnavyoona pichani). Nashukuru Mungu mzigo umekamilika na tayari umeshaanza kwenda hewani kupitia vituo kadhaa vya televisheni. Thanx kwa director wangu, Tonee na jembe lake, Chief bila kuwasahau prodyuza wangu, Mobbyzow wa Bamba Records, Deez, shost wangu Zuhura, dansa wangu MC V na wote walioshiriki kufanikisha mpango huo. Mungu awabariki sana, naombeni sasa tuwaachie kazi Watanzania ambao ndiyo majaji, naamini watatupokea vizuri pamoja na familia tuliyoianzisha, 'BADUGU NATIONAL'
ASANTENI KWA SAPOTI YENU.