"Mambo vipi watu wangu?
Pokeeni video yangu mpya inaitwa Kings & Queens ambayo nimeifanya kupitia Kampuni ya Ogopa video ya Kenya, tayari imeanza kuonekana kunako kituo cha Televisheni cha MTV Base, kabla ya kusambaa ndani ya TV za Bongo.
Ngoma nyingine mpya ambayo nimeachia audio kupitia redio mbalimbali inaitwa BED AND
BREAKFAST iliyotengenezwa katika studio za B.HITZ MUSIC GROUP chini ya
Producer Hermy B. Mastering ikafanyika ndani ya studio ya OGOPA DEE JAYS, Kenya.
Video ya wimbo huu itafanyika mwezi huu ndani ya JOHANNESBURG SOUTH AFRICA,
itagongwa na kampuni bora kabisa AFRICA inayojulikana kwa jina la FILM ONLINE ambayo ilimfanya mwanamuziki kutoka humo, HHP kuchukua tuzo ya BEST
VIDEO MTV 2009.
Lengo kubwa ni kupiga hatua zaidi katika anga za kimataifa na kwenda kwenye level walizokuwa wasanii wengine. Najua yote haya yanafanyika kwa kuwa mnanisupport sana, NAPENDA KUSEMA NAWASHUKURU SANA, MSICHOKE KUNISUPPORT NA SITAWAANGUSHA.
TUFUNGE MWAKA NA KUUANZA MWAKA MPYA WA 2010 NA
MZIGO MPYA KUTOKA KWA MZEE WA COMMERCIAL", A.Y.
MAANDALIZI YA MKUTANO MKUU CCM YASHIKA KASI
9 hours ago
One Responses to "HII NDIYO VIDEO MPYA YA A.Y"