Kutoka Mpanda, Mkoani Rukwa majanki wawili wanaofanya game ya muziki wa Bongo Flava, Gabboman na Side Teacher a.k.a Wana wa Pinda wameibukan na ngoma ya ukweli yenye jina la 'Wana wa Pinda' wakimpa big up Waziri Mkuu, Mizengo Pinda ambaye pia ni Mbunge wao wa Mpanda Mashariki na kuufagilia mkoa wao kwa ujumla. Ishu mpya iliyonidondokea wakati naingiza stori hii hapa ni kwamba ngoma hiyo tayari imeanza kubamba kupitia vituo kadhaa vya redio na kupenya kunako chati za muziki huo. Big Up Wana wa Pinda, mwanzo mzuri, endeleeni kukaza.
Monday, December 28, 2009
Posted in | |
0 Comments »
One Responses to "UNAWAJUA WANA WA PINDA?"