Siku zimesogea na mwisho wa ubishi unakaribia, shindano la kumpata ‘handsome boy’ mwenye jina kubwa nchini, Ijumaa Sexiest Bachelor linaelekea ukingoni na Desemba 20, 2009 ndiyo fainali yenyewe.
Mzigo wa kumpata Ijumaa Sexiest Bachelor 2009, utamalizwa ubishi kwenye Ukumbi wa TCC Club, Chang’ombe, Dar es Salaam ambapo mastaa wanne, waliobaki mmoja wao atakabidhiwa taji.
Mpango kamili utasindikizwa na Bendi ya African Stars ‘Twanga Pepeta International’ ambayo kwa sasa inatawala soko la muziki wa dansi kwa nyimbo zake ziliziopo kwenye chati.
Handsome Boys, Hemed Suleiman, Lawrence Malima ‘Marlaw’, Yusuf Mlela na Steven Kanumba, kati yao ataibuka na taji hilo linaloheshimiwa zaidi na wadau wa burudani nchini.
Steven Kanumba ndiye anayeshikilia taji hilo ambalo alilitwaa mwaka juzi baada ya kumwaga kwenye fainali, golikipa wa Simba, Juma Kaseja kwa kura chache na romantic vocalist wa Bongo Flava, Aboubakar Katwila ‘Q Chillah’.
Ni nani anayedatisha, Hemed, Kanumba, Yusuf au Marlaw? Jibu litapatikana Jumapili ya Desemba 20, ndani ya TCC Club, huku burudani ya kutakata ‘ikifanzwa’ kwa ukamilifu na Twanga.
Ijumaa Sexiest Bachelor, imedhaminiwa na Zizzou Fashion, Dotnata Decoration, African Stars Entertainment Tanzania (ASET) na Sceen Masters.
Bado unaweza kumfanya staa wako ashinde kwa kutuma ujumbe wa simu (SMS), ukiandika nambari yake ya ushiriki kwenda namba 15551.
MAANDALIZI YA MKUTANO MKUU CCM YASHIKA KASI
9 hours ago
One Responses to "MWISHO WA UBISHI IJUMAA SEXIEST B J'2?"