Albamu mpya ya mwana Hip Hop ‘bei mbaya’ Bongo, Joseph Mbilinyi ‘Mr. II’ inayokwenda kwa jina la Veto, tayari imeanza kukubalika, kitaani kutokana na idadi kubwa ya Wamachinga kutoa ripoti chanya kuhusu mauzo.
Akipiga stori na ebwanadaah juzi Sugu alisema kwamba, Wamachinga walioripoti kwake katikati ya wiki iliyopita walisema kuwa jinsi wanavyosumbuliwa mtaani na wadau wa burudani wanaoiulizia Veto, ni wazi kwamba inakubalika, hivyo wengi wanapenda kuipata.
Sugu alisema kuwa ameona Wadosi ambao walikuwa wanauza zamani ni wazinguaji, hivyo ameamua kubadilisha upepo kwa kuuza mwenyewe, akiwatumia Wamachinga nchi nzima ili kupata fedha yenye maelezo halisi.
“Watu wananipigia simu, wananiuliza Veto vipi? Wadosi wanatuumiza, kwahiyo tunasambaza na Wamachinga, kwahiyo popote pale mdau akimuona Mmachinga amwite amuulize Veto, atapata albamu bora ya Hip Hop,” alisema Sugu.
One Responses to "KAMATA VETO YA SUGU KITAANI"