ILI MUZIKI WETU UWEZE KWENDA KIMATAIFA NI LAZIMA TUBADILIKE, SAPOTI YAKO PIA MUHIMU

Hapa nikimkaribisha aliponitembelea ofisini
Zay B akionesha bado yuko gado

Hii ndiyo ndinga yake

Huu ndiyo mjengo wake

Kutoka Bongo mwana Hip Hop wa kike aliyeleta mapinduzi katika game ya muziki wa kizazi kipya kwa upande wa wasichana, Zainabu Lipangile a.k.a Zay B mwishoni mwa wiki iliyopita alidondoka ndani ya blog hii na kupiga stori mbili tatu ikiwemo kutangaza baadhi ya aseti anazomiliki hivi sasa kama alivyofanya Waziri Mkuu, Mhe. Mizengo Pinda.

Zay B alisema kwamba wapo baadhi ya watu wakiwemo wasanii wenzie wamekuwa wakivumisha maneno mitaani kwamba hivi sasa amefulia baada ya kupotea kwenye game kwa muda mrefu kitu ambacho amekikanusha, ndiyo sababu iliyomfanya atangaze mali zake.

“Unajua watu wengine huwa wanakosa ishu za kuongea, mimi kutosikika siyo kwamba nimefulia, kuna ishu kibao nafanya zinazoniingizia kipato, kwanza muziki wa Bongo haulipi na umejaa majungu. Ningekuwa nimefulia ningeweza kujenga nyumba au kununua gari?” Alihoji Zay B huku akionesha picha za nyumba yake zilizokuwa kwenye simu.

Mwanadada huyo alisema kwamba mjengo huo ameushusha pande za Buyuni, Pugu nje kidogo ya Dar es Salaam huku akimiliki gari aina ya Toyota Premio. “Mbali na hayo pia nimesaini mkataba wa kufanya kazi ya muziki na Kampuni ya Butile Africa Group ya Afrika Kusini, watu wasifikiri nipo nipo tu, sijafulia kihiivyo,”.


Tuesday, January 19, 2010 Posted in | | 0 Comments »

One Responses to "ZAY B BADO YUKO GADOOOO!!!"

Write a comment