ILI MUZIKI WETU UWEZE KWENDA KIMATAIFA NI LAZIMA TUBADILIKE, SAPOTI YAKO PIA MUHIMU
Artists wawili wa Muziki wa Kizazi Kipya wenye heshima tele Bongo, Ambwene Yesaya, A.Y na Lawrence Malima Madole a.k.a Marlow, wamekomba tuzo za TEENEZ zilizotolewa pande za Nairobi, Kenya. Aprili 17, mwaka huu.
Story iliyotua kunako blog hii imeweka kweupe kwamba, ishu hiyo ambayo kwa hapa Bongo imekuwa kama ‘sapraizi’ kwakutokuwa na promo ya kutosha ilichukua nafasi pande hizo weekend iliyopita ambapo A.Y aliibuka na ‘awadi’ ya Msanii Bora wa Afrika Mashariki.
Kwa upande wa Marlaw aliondoka na tuzo ya the most downloaded song kupitia ngoma yake ya Pipi.
“Kwangu mimi ni heshima inayoendelea kuwepo, inanipa moyo ili niongeze bidii katika kuandika ngoma kali,” alisema A.Y mbele ya ebwanadaah.
BEST EAST AFRICAN ARTIS CATEGORY:
MARLAW-TANZANIA
WEASEL AND RADIO-UGANDA
AY-TANZANIA
BLU 3-UGANDA
Mchizi kutoka pande za Nigeria, J. Martins anayeendelea kufanya maajabu kunako game ya muziki kupitia ngoma zake kadhaa ikiwemo Iva jana usiku alimaliza kazi iliyomleta Bongo kwa kuangusha burudani ya ukweli ndani ya ukumbi uliyopo kwenye mjengo mpya wa Kampuni ya simu za mkononi ya Zain uliyopo mitaa ya Moroko, Dar.
Kama wewe pia unainjoi kuangalia muvi za komedi kama mimi ni lazima utakuwa umeshaicheki Scooby Doo. Nimevutiwa na picha hii nikaamua kuidondosha hapa.
Read More......The Bongo Hip Hop Legend, Godfrey Tumaini ‘Dudubaya’ amezindua harakati mpya ya kuitetea Hip Hop na Bongo Flava pamoja na wasanii wake kwa kutoa CD inayoelezea kinagaubaga unyonyaji unaoendelea aliyoipa jina la Nguruwe. In that CD, Ze Dudu a.k.a Baba Willy anawachana presenters & DJ’s ambao wanatajwa kuishi kimjini mjini kwa mgongo wa wasanii ambao wanawanyonya.
Mbali na kuwadisi presenters & DJ’s hao, pia Dudu ametoa shut out kwa waandishi na wadau wa burudani Bongo wanaheshimu taaluma kwa kutokuendekeza rushwa.
Kwa sauti kavu, pia Dudu amewagonga nyundo baadhi ya wana Hip Hop wanaojiita wanaharakati kwamba sifa hiyo haiendani nao kwa sababu ni wanyonge na hawajui kutetea haki zao na za muziki huo kwa ujumla.
“Kuna Ma-DJ wamegoma kupiga nyimbo zangu tangu mwaka 2006, miaka minne bado nipo. Sijaenda kuomba msamaha na ninaishi, sisi ndiyo ma-legendary wa huu muziki, tumetoka nao mbali halafu watu wanakuja kula kiulaini.
“Mtu unaimba Hip Hop unajiita mwanaharakati, siku mbili nyimbo zako hazichezwi redioni unakwenda kuomba msamaha, unapiga magoti,” Ze Dudu anasikika akigonga sauti ndani ya CD hiyo.
Akichambua umafia wa baadhi ya watangazaji na Ma-DJ Bongo, Ze Dudu anamwaga kuwa kuna watu wameweka mkakati kwamba bila shilingi 500,000 hawaruhusu kupiga nyimbo redioni kitu ambacho ni sawa na unyonyaji.
“Hizo laki tano tano msanii atatoa kwa redio ngapi? Kwa uwezo upi? Halafu unatengeneza albamu kwa milioni 4, unakwenda kwa mdosi unalipwa milioni 2, msanii atapata nini?” Anahoji Ze Dudu na kuongeza:
“Mtangazaji anakupigia simu anakuuliza upo wapi? Unamjibu upo baa, baada ya dakika chache anakuja na wapambe, demu wake, wanaagiza vinywaji vya bei mbaya eti ‘bili’ yote juu yako msanii. Watu tuna familia, mimi mwanangu Willy anasoma International School.”
"Baada ya stori hiyo yenye jina la Nguruwe pati one, inakuja pati two yake ambayo naifanya na vichwa kama Mkoloni wa Wagosi wa Kaya na Afande Sele, tunataka kuwaambia ukweli wale wanaotaka kujinufaisha kupitia migongo yetu," alisema Dudu alipoongea na ebwanadaah..
Baada ya kufanya vyema na kazi yenye jina la Nipe ripoti akiwa na Spark, Tundaman kutoka ndani ya familia ya Tip Top Connection amesimama tena na ngoma mpya yenye jina la Hali yangu mbaya akiwashirikisha Madee na Chegge wa Kiumeni. Ebwanadah inakupa shavu la kutosha kijana kwa kuendelea kukaza kunako game hiyo.
Read More......KARIBU SANA
JE, WEWE NI MJANJA?
UNAJUA KUDANSI?
SHOUT OUT !!
Followers
My Blog List
-
-
-
-
SIMBA SC. YAWEKA SOKONI MAJI YAKE!8 years ago
-
-
HARD PRICE COMING SOON10 years ago
-
-
-
Aslay Akifanya Vitu vyake13 years ago
-
-
-
-