ILI MUZIKI WETU UWEZE KWENDA KIMATAIFA NI LAZIMA TUBADILIKE, SAPOTI YAKO PIA MUHIMU

Mkoloni, Ze Dudu na Afande Sele

The Bongo Hip Hop Legend, Godfrey Tumaini ‘Dudubaya’ amezindua harakati mpya ya kuitetea Hip Hop na Bongo Flava pamoja na wasanii wake kwa kutoa CD inayoelezea kinagaubaga unyonyaji unaoendelea aliyoipa jina la Nguruwe. In that CD, Ze Dudu a.k.a Baba Willy anawachana presenters & DJ’s ambao wanatajwa kuishi kimjini mjini kwa mgongo wa wasanii ambao wanawanyonya.

Mbali na kuwadisi presenters & DJ’s hao, pia Dudu ametoa shut out kwa waandishi na wadau wa burudani Bongo wanaheshimu taaluma kwa kutokuendekeza rushwa.

Kwa sauti kavu, pia Dudu amewagonga nyundo baadhi ya wana Hip Hop wanaojiita wanaharakati kwamba sifa hiyo haiendani nao kwa sababu ni wanyonge na hawajui kutetea haki zao na za muziki huo kwa ujumla.

“Kuna Ma-DJ wamegoma kupiga nyimbo zangu tangu mwaka 2006, miaka minne bado nipo. Sijaenda kuomba msamaha na ninaishi, sisi ndiyo ma-legendary wa huu muziki, tumetoka nao mbali halafu watu wanakuja kula kiulaini.

“Mtu unaimba Hip Hop unajiita mwanaharakati, siku mbili nyimbo zako hazichezwi redioni unakwenda kuomba msamaha, unapiga magoti,” Ze Dudu anasikika akigonga sauti ndani ya CD hiyo.

Akichambua umafia wa baadhi ya watangazaji na Ma-DJ Bongo, Ze Dudu anamwaga kuwa kuna watu wameweka mkakati kwamba bila shilingi 500,000 hawaruhusu kupiga nyimbo redioni kitu ambacho ni sawa na unyonyaji.

“Hizo laki tano tano msanii atatoa kwa redio ngapi? Kwa uwezo upi? Halafu unatengeneza albamu kwa milioni 4, unakwenda kwa mdosi unalipwa milioni 2, msanii atapata nini?” Anahoji Ze Dudu na kuongeza:

“Mtangazaji anakupigia simu anakuuliza upo wapi? Unamjibu upo baa, baada ya dakika chache anakuja na wapambe, demu wake, wanaagiza vinywaji vya bei mbaya eti ‘bili’ yote juu yako msanii. Watu tuna familia, mimi mwanangu Willy anasoma International School.”

"Baada ya stori hiyo yenye jina la Nguruwe pati one, inakuja pati two yake ambayo naifanya na vichwa kama Mkoloni wa Wagosi wa Kaya na Afande Sele, tunataka kuwaambia ukweli wale wanaotaka kujinufaisha kupitia migongo yetu," alisema Dudu alipoongea na ebwanadaah..


Friday, April 16, 2010 Posted in | | 0 Comments »

One Responses to "ZE DUDU NA MA-DJ 'NGURUWE'"

Write a comment