Artists wawili wa Muziki wa Kizazi Kipya wenye heshima tele Bongo, Ambwene Yesaya, A.Y na Lawrence Malima Madole a.k.a Marlow, wamekomba tuzo za TEENEZ zilizotolewa pande za Nairobi, Kenya. Aprili 17, mwaka huu.
Story iliyotua kunako blog hii imeweka kweupe kwamba, ishu hiyo ambayo kwa hapa Bongo imekuwa kama ‘sapraizi’ kwakutokuwa na promo ya kutosha ilichukua nafasi pande hizo weekend iliyopita ambapo A.Y aliibuka na ‘awadi’ ya Msanii Bora wa Afrika Mashariki.
Kwa upande wa Marlaw aliondoka na tuzo ya the most downloaded song kupitia ngoma yake ya Pipi.
“Kwangu mimi ni heshima inayoendelea kuwepo, inanipa moyo ili niongeze bidii katika kuandika ngoma kali,” alisema A.Y mbele ya ebwanadaah.
BEST EAST AFRICAN ARTIS CATEGORY:
MARLAW-TANZANIA
WEASEL AND RADIO-UGANDA
AY-TANZANIA
BLU 3-UGANDA
One Responses to "A.Y, MARLAW NA TUZO ZA KIMYAKIMYA"