ILI MUZIKI WETU UWEZE KWENDA KIMATAIFA NI LAZIMA TUBADILIKE, SAPOTI YAKO PIA MUHIMU

Jana jioni mwanadada Zainabu Lipangile a.k.a Zay B alinitumia ujumbe mfupi wa maandishi (SMS) akionesha kuguswa na tuzo za muziki, Kili 2009-2010. Nami naudondosha kwenu kama ifuatavyo yakiwa ni maoni yake.
"Kili Music Awards kwanini wasanii wa kike tunaofanya muziki wa Hip Hop hawatupi nafasi ya kushiriki? Kila mwaka wanatutenga, category zote ziko wanawake na wanaume kasoro Hip Hop.
Unajua tuzo ni heshima na silazima apewe Zay B ila tufikiriwe, suala la kusema wasanii wa kike wachache si kweli, tuko zaidi ya watano ambao ni maarufu, siyo kwangu ishu kupewa tuzo, ila acheni ubaguzi. Mimi ni Mama Afrika mtetezi wa wanawake, tupeni haki yetu".

Sunday, April 18, 2010 Posted in | | 0 Comments »

One Responses to "SMS KUTOKA KWA ZAY B KUHUSU KILI AWARDS"

Write a comment