ILI MUZIKI WETU UWEZE KWENDA KIMATAIFA NI LAZIMA TUBADILIKE, SAPOTI YAKO PIA MUHIMU

Mfanyakazi wa maduka ya Zizzou Fashion, Waiya akikabidhi mifuko yenye pamba kwa Mlela huku mimi (katikati) nikishuhudia.
Na pia nilipata chansi ya 'kushoolavu' na sista Waiya

Ijumaa Sexiest Bachelor, Yusuf Mlela jana alikabidhiwa zawadi zake ambazo ni pamba zenye thamani ya shilingi laki 5 kutoka kwa mdhamini wa shindano hilo, maduka ya Zizzou Fashion.

Read More......
Wednesday, December 30, 2009 Posted in | | 0 Comments »

Siku kadhaa baada ya Yusuf Mlela kuibuka na ushindi wa Ijumaa Sexiest Bachelor, nilikutana naye na kugonga photo za kumbukumbu, huku picha zake nyingine tukizitumia katika magazeti yetu ikiwa ni ahadi tuliyomuahidi ya kumtangaza kama mshindi mpaka atakapolivua taji hilo.

Read More......
Monday, December 28, 2009 Posted in | | 0 Comments »

Mimi na mshikaji wangu, Walter a.k.a Ota 'tukishoo lavu' na tuzo ya Gazeti la Championi iliyopata kutoka kwa waandaaji wa Kombe wa Dunia 2010 huko Sauzi kupitia kwa Mhariri wake mtendaji, Salehe Ally

Read More......
Posted in | | 0 Comments »

Mimi, Maimatha wa Jese na Malotto tukizindua tuzo

Sugu akimkabidhi Yusuf Mlela tuzo ya ushindi

Mlela mara baada ya kutangazwa mshindi na kukabidhiwa tuzo na Sugu

Kanumba akiwa na cheti za uthibitisho wa kushiriki
Dada wa Hemed Suleiman alichukua cheti kwa niaba yake
Luqman, Da Asha, Shaluwa na mimi, tukipozi baada ya shoo

Read More......
Posted in | | 0 Comments »

Side Teacher na Gabboman katika pozi
Kutoka Mpanda, Mkoani Rukwa majanki wawili wanaofanya game ya muziki wa Bongo Flava, Gabboman na Side Teacher a.k.a Wana wa Pinda wameibukan na ngoma ya ukweli yenye jina la 'Wana wa Pinda' wakimpa big up Waziri Mkuu, Mizengo Pinda ambaye pia ni Mbunge wao wa Mpanda Mashariki na kuufagilia mkoa wao kwa ujumla. Ishu mpya iliyonidondokea wakati naingiza stori hii hapa ni kwamba ngoma hiyo tayari imeanza kubamba kupitia vituo kadhaa vya redio na kupenya kunako chati za muziki huo. Big Up Wana wa Pinda, mwanzo mzuri, endeleeni kukaza.

Read More......
Posted in | | 0 Comments »


Umetuona?
Siku hiyo Brian aliinjoi ile mbaya

Jumamosi moja iliyopita, majira ya mchana nilimtoa out baby wangu, Brian kwenye tamasha moja maalum kwa ajili yao (Baby Canival) lililoandaliwa na Kampuni ya MultChoice kwenye viwanja vyao vilivyopo pande za Oysterbay. Huko nilikutana na Eliza tukabadilishana mawili matatu ikiwemo kumpa big up kwa hatua aliyofikia ndani ya mjengo wa BBA Revolution.

Read More......
Posted in | | 0 Comments »



KUMBUKUMBU

Leo Ijumaa, Desemba 18, 2009 ni mwaka mmoja tangu
Mama yetu mpendwa LIDYA ANANIA YESSAYAH
alipotutoka ghafla hapa Duniani na
kutuachia pengo lisilozibika katika Familia.
Japokuwa haupo nasi hapa duniani lakini
tupo nawe Kiroho kwa kuendeleza mema yote uliyotufundisha na
kutuasa.Tunakukumbuka kwa Upendo,
Busara na Ukarimu uliokuwa nao kwa familia na marafiki.
Daima unakumbukwa sana na watoto wako
wapendwa John, Summa, Ambwene na
Mage..Unakumbukwa na Baba yako, ndugu
zako, washarika, majirani, jamaa na
marafiki zako wote.

MSHUKURUNI BWANA KWA KUWA NI MWEMA KWA
MAANA FADHILA ZAKE NI ZA MILELE.

(Ufunuo 14:13)


























Read More......
Friday, December 18, 2009 Posted in | | 0 Comments »

"Mambo vipi watu wangu?
Pokeeni video yangu mpya inaitwa Kings & Queens ambayo nimeifanya kupitia Kampuni ya Ogopa video ya Kenya, tayari imeanza kuonekana kunako kituo cha Televisheni cha MTV Base, kabla ya kusambaa ndani ya TV za Bongo.
Ngoma nyingine mpya ambayo nimeachia audio kupitia redio mbalimbali inaitwa BED AND
BREAKFAST iliyotengenezwa katika studio za B.HITZ MUSIC GROUP chini ya
Producer Hermy B. Mastering ikafanyika ndani ya studio ya OGOPA DEE JAYS, Kenya.
Video ya wimbo huu itafanyika mwezi huu ndani ya JOHANNESBURG SOUTH AFRICA,
itagongwa na kampuni bora kabisa AFRICA inayojulikana kwa jina la FILM ONLINE ambayo ilimfanya mwanamuziki kutoka humo, HHP kuchukua tuzo ya BEST
VIDEO MTV 2009.
Lengo kubwa ni kupiga hatua zaidi katika anga za kimataifa na kwenda kwenye level walizokuwa wasanii wengine. Najua yote haya yanafanyika kwa kuwa mnanisupport sana, NAPENDA KUSEMA NAWASHUKURU SANA, MSICHOKE KUNISUPPORT NA SITAWAANGUSHA.
TUFUNGE MWAKA NA KUUANZA MWAKA MPYA WA 2010 NA
MZIGO MPYA KUTOKA KWA MZEE WA COMMERCIAL", A.Y.

Read More......
Posted in | | 0 Comments »




- Aina ya Gari ni SUZUKI AERIO
- Mwaka 2001
- Imetembea 69000 kms
- Bei Milioni 14
- Full music with air condition [A/C] and srs (airbag)
- Automatic transmission
- Mawasiliano: 0715 588181, 0784 588181

Read More......
Posted in | | 0 Comments »

Siku zimesogea na mwisho wa ubishi unakaribia, shindano la kumpata ‘handsome boy’ mwenye jina kubwa nchini, Ijumaa Sexiest Bachelor linaelekea ukingoni na Desemba 20, 2009 ndiyo fainali yenyewe.
Mzigo wa kumpata Ijumaa Sexiest Bachelor 2009, utamalizwa ubishi kwenye Ukumbi wa TCC Club, Chang’ombe, Dar es Salaam ambapo mastaa wanne, waliobaki mmoja wao atakabidhiwa taji.
Mpango kamili utasindikizwa na Bendi ya African Stars ‘Twanga Pepeta International’ ambayo kwa sasa inatawala soko la muziki wa dansi kwa nyimbo zake ziliziopo kwenye chati.
Handsome Boys, Hemed Suleiman, Lawrence Malima ‘Marlaw’, Yusuf Mlela na Steven Kanumba, kati yao ataibuka na taji hilo linaloheshimiwa zaidi na wadau wa burudani nchini.
Steven Kanumba ndiye anayeshikilia taji hilo ambalo alilitwaa mwaka juzi baada ya kumwaga kwenye fainali, golikipa wa Simba, Juma Kaseja kwa kura chache na romantic vocalist wa Bongo Flava, Aboubakar Katwila ‘Q Chillah’.
Ni nani anayedatisha, Hemed, Kanumba, Yusuf au Marlaw? Jibu litapatikana Jumapili ya Desemba 20, ndani ya TCC Club, huku burudani ya kutakata ‘ikifanzwa’ kwa ukamilifu na Twanga.
Ijumaa Sexiest Bachelor, imedhaminiwa na Zizzou Fashion, Dotnata Decoration, African Stars Entertainment Tanzania (ASET) na Sceen Masters.
Bado unaweza kumfanya staa wako ashinde kwa kutuma ujumbe wa simu (SMS), ukiandika nambari yake ya ushiriki kwenda namba 15551.

Read More......
Tuesday, December 15, 2009 Posted in | | 0 Comments »

Fid na Matonya katika pozi

Ishu mpya iliyodondoka ndani ya ebwanadaah hivi punde zinatapakaa kwamba wakali kibao wa muziki wa Bongo Flava wanatarajia kudondoka pande za Iringa kwa ajili ya shughuli moja tu, tamasha kubwa lenye jina la MITIKISIKO.
Mratibu wa ishu hiyo, Edwin a.k.a Eddo wa Redio Ebony FM ya huko aliwataja wakali hao kuwa ni Fid Q, Matonya, Squezeer, Chegge, Madee, Tundaman, Blue, Baby Madaha, Linex, Nay wa Mitego, Dully, Felly na wengine kibao huku wale wapenzi wa mirindimo ya pwani wakirusha vidole juu na kundi la Coast Morden taarabu bila kuisahau bendi kali ya Sweat Noise ya Iringa.
"Pia kutakuwa na mchezo wa masumbwi kati ya mkali Rashid Matumla na 'Snake Boy' na Chupaki wa Iringa. Ishu zote hizo zitagongwa ndani ya Uwanja wa mpira wa Samora, Desemba 6, kuanzia saa sita mchana mpaka saa 12 jioni chini ya udhamni wa Kampuni ya simu za mkononi, Vodacom. Ni zaidi ya burudani," alisema Eddo.

Read More......
Sunday, November 29, 2009 Posted in | | 0 Comments »

Safu maarufu ya Mpaka Home inayopatikana ndani ya Gazeti la Risasi, J'5, Nov 23, 2009 ilitimiza umri wa miaka minne, sherehe fupi ya Birthday hiyo ilifanyika Ijumaa ya wiki iliyopita katika ofisi zetu zilizopo Sinza, Bamaga, Dar es Salaam. Baadhi ya mastaa wa Bongo waliyowahi kutembelewa na Mpaka Home walikuwa ni miongoni mwa wageni waalikwa katika tafrija hiyo fupi. Hebu cheki tulivyoinjoi.

Mhariri Mtendaji wa Magazeti ya Global Publishers, Richard Manyota aliibariki hafla hiyo kabla ya kuanza rasmi
Nikiwa kama muasisi wa Mpaka Home niliwaeleza wageni waalikwa historia fupi ya safu hiyo
Mkubwa Fella kama mgeni mualikwa alikuwa wa kwanza kutoa maoni yake kuhusiana na Mpaka Home
Akafuata 'Rais' wa Manzese Madee
Kanumba pia alikuwa na machache ya kuongea
Yusuf Mlela naye alisema kitu kuhusu kuiboresha zaidi Mpaka Home
Frola Mvungi wa Bongo Dar es Salaam aliwawakilisha mastaa wa kike katika hafla hiyo
Ray pia alitupa maoni yake mazuri
Kutoka Tip Top Connection, Tundaman naye aliongea
Hatimaye ulifika ule wakati muafaka, siunaona kitu cha keki?
Mimi ndiye nilikuwa wa kwanza kulishwa na Imelda Mtema wa Mpaka Home ambaye kwa pamoja tumeifanya safu hii kuwa juu.
Mimi pia nilifanya hivyo kwake

Akafuata Ray
Yusuf Mlela
Madee
Kanumba
Frola Mvungi
George Kayala (Mhariri msaidizi wa Gazeti la Risasi)
Mhariri wa Gazeti la Ijumaa ambaye pia alikuwa muendesha shughuli wetu siku hiyo, Amrani Kaima naye alikamua keki
Mhariri wa Gazeti la Ijumaa Wikienda na mshauri mkuu wa Mpaka Home, Luqman Maloto naye pia alipata heshima hiyo
Mara ikafika zamu ya msanifu kurasa msaidizi wa Mpaka Home, Walter a.k.a Ota
Mimi pia nilihusika kumlisha keki, mshauri mwingine wa Mpaka Home, Hamida Hassan a.k.a Sista Doi.
Hapa nikimlisha msanifu kurasa chipukizi wa magazeti ya Global, Frank
Ilifika zamu ya dada Glory ambaye ni secretary wetu ofisini
Mfanyakazi mwenzetu, Ally Mbetu naye aliinjoi kwa kitu cha keki
Mara ikafika zamu ya Aloyce ambaye ni mchoraji kwenye magazeti yetu
Kilichofuata baada ya keki zilikuwa ni picha za pozi kwa ajili ya kumbukumbu
Hapa nimetulia na Kanumba katika pozi la kipole zaidi
Hapa nikitabasamu na Ray
Ray, Imelda wa Mpaka Home na Kanumba
Mwisho niliwashukuru wageni kwa kukubali mwaliko wetu na wote waliyofanikisha hafla hiyo kuwa juu. Wapenzi wasomaji wa Mpaka Home miaka hiyo minne kwetu ni kama changamoto ya kufanya mambo makubwa zaidi ili nyinyi mpate kuinjoi na kufahamu maisha halisi ya mastaa wenu wa Kibongo.

Read More......
Posted in | | 0 Comments »