ILI MUZIKI WETU UWEZE KWENDA KIMATAIFA NI LAZIMA TUBADILIKE, SAPOTI YAKO PIA MUHIMU

Safu maarufu ya Mpaka Home inayopatikana ndani ya Gazeti la Risasi, J'5, Nov 23, 2009 ilitimiza umri wa miaka minne, sherehe fupi ya Birthday hiyo ilifanyika Ijumaa ya wiki iliyopita katika ofisi zetu zilizopo Sinza, Bamaga, Dar es Salaam. Baadhi ya mastaa wa Bongo waliyowahi kutembelewa na Mpaka Home walikuwa ni miongoni mwa wageni waalikwa katika tafrija hiyo fupi. Hebu cheki tulivyoinjoi.

Mhariri Mtendaji wa Magazeti ya Global Publishers, Richard Manyota aliibariki hafla hiyo kabla ya kuanza rasmi
Nikiwa kama muasisi wa Mpaka Home niliwaeleza wageni waalikwa historia fupi ya safu hiyo
Mkubwa Fella kama mgeni mualikwa alikuwa wa kwanza kutoa maoni yake kuhusiana na Mpaka Home
Akafuata 'Rais' wa Manzese Madee
Kanumba pia alikuwa na machache ya kuongea
Yusuf Mlela naye alisema kitu kuhusu kuiboresha zaidi Mpaka Home
Frola Mvungi wa Bongo Dar es Salaam aliwawakilisha mastaa wa kike katika hafla hiyo
Ray pia alitupa maoni yake mazuri
Kutoka Tip Top Connection, Tundaman naye aliongea
Hatimaye ulifika ule wakati muafaka, siunaona kitu cha keki?
Mimi ndiye nilikuwa wa kwanza kulishwa na Imelda Mtema wa Mpaka Home ambaye kwa pamoja tumeifanya safu hii kuwa juu.
Mimi pia nilifanya hivyo kwake

Akafuata Ray
Yusuf Mlela
Madee
Kanumba
Frola Mvungi
George Kayala (Mhariri msaidizi wa Gazeti la Risasi)
Mhariri wa Gazeti la Ijumaa ambaye pia alikuwa muendesha shughuli wetu siku hiyo, Amrani Kaima naye alikamua keki
Mhariri wa Gazeti la Ijumaa Wikienda na mshauri mkuu wa Mpaka Home, Luqman Maloto naye pia alipata heshima hiyo
Mara ikafika zamu ya msanifu kurasa msaidizi wa Mpaka Home, Walter a.k.a Ota
Mimi pia nilihusika kumlisha keki, mshauri mwingine wa Mpaka Home, Hamida Hassan a.k.a Sista Doi.
Hapa nikimlisha msanifu kurasa chipukizi wa magazeti ya Global, Frank
Ilifika zamu ya dada Glory ambaye ni secretary wetu ofisini
Mfanyakazi mwenzetu, Ally Mbetu naye aliinjoi kwa kitu cha keki
Mara ikafika zamu ya Aloyce ambaye ni mchoraji kwenye magazeti yetu
Kilichofuata baada ya keki zilikuwa ni picha za pozi kwa ajili ya kumbukumbu
Hapa nimetulia na Kanumba katika pozi la kipole zaidi
Hapa nikitabasamu na Ray
Ray, Imelda wa Mpaka Home na Kanumba
Mwisho niliwashukuru wageni kwa kukubali mwaliko wetu na wote waliyofanikisha hafla hiyo kuwa juu. Wapenzi wasomaji wa Mpaka Home miaka hiyo minne kwetu ni kama changamoto ya kufanya mambo makubwa zaidi ili nyinyi mpate kuinjoi na kufahamu maisha halisi ya mastaa wenu wa Kibongo.

Sunday, November 29, 2009 Posted in | | 0 Comments »

One Responses to "MIAKA 4 YA MPAKA HOME, FULL FURAHA"

Write a comment