Kutoka pande za Tip Top, Manzese, Dar es Salaam ebwanadaah ilipata kupiga stori mbili tatu na ‘Rais’ wao Hamad Ally a.k.a Madee ishu kubwa ikiwa ni uvumi ulioenea na kuripotiwa na chombo kimoja cha habari kwamba, jamaa hajaachana na demu wake wa siku nyingi, Pendo kama alivyoimba kwenye ngoma yake ya Pesa kuwa, binti kamtosa kwasababu hana mkwanja.
Kwa upande wake Madee alisema kwamba, yeye hana taarifa na uvumi huo na kwamba alichokiimba kwenye wimbo wake wa Pesa ndiyo ukweli na hana mpango wa kurudiana na Pendo kwakuwa tayari ameshasahau yote yaliyopita na kuganga yajayo.
“Wewe MC George ni kama ndugu yangu, sioni sababu ya kukuficha kuhusu hilo, Pendo mimi siko naye na nilichokiimba ndiyo ukweli wenyewe, kama kuna chombo cha habari kimeandika kuhusu hilo inawezekana wameongea na yeye lakini kwa upande wangu najua tumeshaachana siku nyingi,” alisema Madee.
Akiuzungumzia wimbo mmoja wa Bongo Flava ambao jina na wasanii walioimba hawajafahamika bado unaopinga kuwepo kwa Rais wa Manzese, Madee alisema na ebwanadaah kwamba yeye atabaki kuwa rais wa pande hizo tena wa milele kwani ndiye msanii anayetambulisha vyema maeneo hayo na hata kama watatokea wachache wanaompinga wengi watamsapoti.
“Kama wao wamegoma kunipa kura, kaka zao, dada zao na ndugu zao wengine wamenipa kura na ndiyo maana karibu mikoa yote ninayoenda kufanya shoo wananitambua kama ‘Rais’ wa Manzese, siwezi kushangaa kwakuwa rais lazima awe na wapinzani,” alisema Madee.

Thursday, November 12, 2009
Posted in | |
0 Comments »
One Responses to "MADEE: SIKO NA PENDO JAMANI"