Mabibi na Mabwana kupitia hapa ebwanadaah nachukua fulsa hii kumtambulisha rasmi kwenu kijana kutoka pande za Tanga a.k.a TA, aliyeingia kunako mapambano dhini ya Ufisadi kupitia ngoma zake, Tanzania na Mr. President iliyoanza kusikika wiki mbili zilizopita.
Akiwa anagonga kazi zake kupitia lebo ya Tongwa Records, mchizi anakwenda kwa jina la R.O.M.A ambayo ni a.k.a jina ambalo limetokana na herufi za mwanzo za ndugu zake wanne waliyomtangulia kuzaliwa katika familia yao. Akiwa anapiga buku ndani ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam hivi sasa mchizi anasema kwamba hali duni waliyonayo Wabongo wengi inampa changamoto ya kuandika na kuzishusha hisia zake kupitia mashairi.
"Ngoma zangu zinalenga kuwatetea watu wa chini hasa waishio mikoani ambao wengi wao huishi kwa mlo mmoja kwa siku wakati wapo vigogo ambao wanamiliki mali nyingi kupitia migongo ya jamii hiyo isiyokuwa na uwezo. Kabla sijachia Mr. President hewani niliandika maneno makali sana kwa uchungu niliokuwa nao, lakini baada ya baadhi ya wadau kuisikiliza kazi hiyo walinishauri nipunguze jazba kwa kuondoka maneno makali mpaka ngoma ikawa fresh na kwenda redioni," alisema R.O.M.A.
Ebwanadaah inampa big up za kutosha mchizi kwakuwa ni miongoni mwa wasanii wachache wanaofanya Hip Hop ya ukweli. Mengi zaidi kuhusu R.O.M.A endelea kuchungulia blog hii yenye ishu za ukweli.

Thursday, November 12, 2009
Posted in | |
0 Comments »
One Responses to "HUYU NDIYE R.O.M.A HALISI WA MR. PRESIDENT"