Huwezi amini, lakini ukweli ni kwamba mwana Bongo Flava, Ramadhani Kasembe a.k.a Dullayo Ijumaa ya wiki iliyopita alinusurika kifo baada ya kuchomwa kisu na watu wasiyojulikana kabla ya kudondoka pande za Amana Hospitali na kushonwa nyuzi kumi mkononi.
"Nilikuwa natoka kwenye Klabu moja iliyopo pande za Uwanja wa ndege majira ya saa 10 alfajiri, nikachukua taksi ini-rush home, kabla gari haijaondoka mara washikaji wawili na demu moja wakavamia ndani ya taksi hiyo na kumuamuru dereva awapeleke wanapotaka wao kitu ambacho mimi nilikipinga, baada ya kubishana kwa muda mmoja alishuka akaja upande wangu na kuanza kunipiga na kisu mfululizo, nilikwepa lakini baadae nikaamua kukimamata ndipo alipofanikiwa kunikata mkononi mara mbili," alisema Dullayo alipopiga stori na ebwanadaah!
Mchizi amesema kwamba baada ya kukatwa na kisu ilibidi ashuke kwenye gari hiyo kitendo kilichowapa nafasi watuhumiwa, wakamtishia dereva kwa kisu hicho ikabidi aondoe gari kwa kasi na kutokomea kusikojulikana. Baada ya hapo msanii huyo alitafuta usafiri mwingine mpaka katika Hospitali ya Amana ambapo alishonwa nyuzi kumi na kuruhusiwa kurudi home. "Mpaka sasa kesi ipo katika kituo cha polisi Sitakishari, Ukonga, Dar es Salaam tunaendelea kuwasaka watuhumiwa," alisema.
ebwanadaah! inatoa pole nyingi kwa Dullayo na kumtakia afya njema, kwani yote hayo yatapita na mchizi atarudi na kuendelea kuipandisha juu game ya muziki wa kizazi kipya.
HAKI YA WATUMIAJI WA HUDUMA KUADHIMISHWA MACHI 15
11 hours ago
One Responses to "EBWANA DAAH! DULLAYO APIGWA KISU!"