Wakati makundi mawili yaliyoungana kuangusha burudani, TMK Wanaume Family na Tip Top Connection yakiendelea kufanya maajabu katika shoo zake pale yalipodondoka pande za Vavy, Kigamboni mwishoni mwa wiki iliyopita na kufunika mbaya, misiba imeendelea kuchukua nafasi kunako mradi wa muziki wa kizazi kipya.
Mmoja wa wasanii waliyopo katika muungano huo, Amani James Temba a.k.a Mh. Temba katikati ya wiki iliyopita alifiwa na shangazi yake kitu kilichomfanya awe ndani ya wakati mgumu ukizingatia kwamba kifo hicho kilitokea Wilayani Moshi, Kilimanjaro huku yeye akiwa Dar es Salaam anapoishi.
Akipiga stori na safu hii ndani ya ufukwe wa Navy, Kigamboni walipokuwa wakifanya shoo, Temba alisema kwamba, msiba huo ni pigo kwake na kwa ndugu zake wengine kwani Shangazi yake huyo alikuwa na mchango mkubwa ndani ya familia yao. “Yaani hapa nilipo niko safarini, baada ya shoo usiku huu naondoka kuelekea Moshi kwa ajili ya kuwahi mazishi,” alisema Temba.
Msanii huyo alisema kwaba kutokana na ubize aliokuwa nao kunako game yake ya muziki alishindwa kuhudhuria kwenye misimba mingi iliyowahi kutokea kwenye familia yao lakini huu wa sasa hada budi kuhudhuria na kuungana na wanafamilia wengine katika majonzi.
Mbali na Temba, msanii mwinhine wa muziki huo aliyekumbwa na msiba hivi karibuni ni Mandojo abaye alifiwa na baba yake mzazi. Uwazi ShowBiz inawapa pole wasanii hao, yote hayo ni mapenzi yake Mungu, yatapita.
MAANDALIZI YA MKUTANO MKUU CCM YASHIKA KASI
9 hours ago
One Responses to "TEMBA APATA MSIBA"