Makundi mawili yaliyoungana kwa ajili ya kuangusha burudani, TMK Wanaume family na Tip Top Connection yaliendelea kuongeza idadi ya shoo zilizofanya vyema pale yalipovamia ndani ya Ufukwe wa Nevy Beach, Kigamboni, Dar es Salaam jana Ijumaa na kugonga shoo ya kijanja.
Shoo hiyo ambayo iliandaliwa kwa ushirikiano mzuri na kituo cha Redio Magic FM kupitia kipindi chake cha Kwetu Flava, iliwashirikisha pia baadhi ya wakali wa Bongo Flava kama Nay wa Mitego, Kimbunga, Mbishi Real, O-Ten na wengine kibao.
"Baada ya kuzunguka sehemu mbalimbali ndani na nje ya Bongo kwa kazi hiyo, sasa tumerudi home (Dar es salaam), kinachofuata ni kazi kwa kwenda mbele," alisema Fella.
Saturday, November 14, 2009
Posted in | |
0 Comments »
One Responses to "TMK & TIP TOP WAFUNIKA TENA KIGAMBONI"