Wakiwa njiani kuelekea Kanda ya Ziwa walishuka katika kijiji kimoja na kushoo lavu na madenti wa pande hizo.
Walipofika pande za Shinyanga, mkuu wa wilaya hiyo (katikati) aliwaibukia sehemu waliyofikia na kuwapa hi, ikiwa ni pamoja na kuwaasa kuhusiana na gonjwa hatari la Ukimwi
Makundi mawili yaliyoungana pamoja na kupiga kazi kunako mradi wa muziki wa kizazi kipya, TMK Wanaume Family na Tip top Connection mwishoni mwa wiki iliyopita walifunga ukurasa baada ya kumaliza kazi ya kuzunguka katika Mikoa mbalimbali nchini na kuangusha burudani za ukweli.
Akipiga stori na ebwana daah! kwa njia ya simu meneja wa kundi la TMK, Said Hassan Fella alisema kwamba baada ya ziara ndefu iliyoanzia pande za Tabora, Kahama, Geita, Mwanza mjini, Sengerema, Chato na Kakola hatimaye wamemaliza kazi kwa shoo ya ukweli iliyofanyika mjini Bukoba ndani ya Uwanja wa Kaitaba na baadaye Linas Klabu.
"Tunawashukuru wote waliyotusapoti mpaka kufanikisha zoezi hilo bila kuwasahau mashabiki wetu, tunarudi Dar kujipanga kwa ajili ya kuendelea na ishu nyingine," alisema Fella.
Monday, November 2, 2009
Posted in | |
0 Comments »
One Responses to "TMK, TIP TOP WAMALIZA KAZI BUKOBA"