Bendi ya muziki wa dansi, Akudo Impact imejiandaa kuukabili mwaka 2011 kwa kuimarisha safu ya uongozi na baadhi ya mabadiliko ambayo yatawafanya kusimama vyema kwa msimu ujao.
Akipiga stori na ebwanadaah juzi, George J. Kyatika ambaye ni afisa uhusiano mpya wa bendi hiyo alisema kwamba AKUDO ni moja ya bendi za muziki wa dansi nchini ambazo zimefanikiwa na kuweka historia ya kipekee katika nyanja ya burudani. Kwa kutambua hilo juhudi binafsi zinafanyika kuhakikisha heshima hiyo haitoweki wala kupungua bali kukuzwa na kuongezeka maradufu.
"Tayari tumejipanga upya kuja na albamu nyingine iliyosheheni nyimbo zitakazosisimua na kuwagusa vilivyo wapenzi na mashabiki wa muziki. Baada ya kusema hayo naomba niitambulishe safu nyingine ya uongozi ambayo ni ndugu Gabriel J. Kisanga ambaye ni Meneja Masoko. Pia nawafahamisha kuwa rapa wetu Canal Top amerudi nyumbani, baada ya kusemwa mengi kuhusu kuhama kwake" alisema George.
Ifuatanyo chini ni ratiba ya shoo za Akudo Impact kwa mwezi huu wa Desemba.
11/12 JUMAMOSI KIGAMBONI
12/12 JUMAPILI MSASANI BEACH
17/12 IJUMAA MANGO GARDEN
18/12 JUMAMOSI FK KIMARA TEMBONI
19/12 JUMAPILI MSASANI
24/12 IJUMAA VIGAE CLASSIC
25/12 JUMAMOSI MSASANI BEACH
26/12 JUMAPILI MSASANI BEACH
29/12 JUMATANO CLUB SUNSIRO
31/12 IJUMAA MANGO GARDEN
One Responses to "AKUDO IMPACT YABADILI UONGOZI, KANAL TOP NDANI"