Memba wa kundi lililowahi kufanya vyema katika game ya muziki wa Bongo Flava kwenye miaka ya 2000, BWV lenye maskani yake pande za Mwanza, Hamad Salehe 'Cool D' (aliyechuchumaa pichani juu) amefariki dunia jana na kuzikwa leo kwenye makaburi Kirumba huko huko Rock City.
Akipiga stori na ebwanadaah aliyekua kiongozi wa kundi hilo ambaye hivi sasa ni mtangazaji wa kituo cha Redio Passion FM, Phillibert Kabago alisema kuwa mshikaji alikuwa akisumbuliwa na maradhi kwa muda wa wiki kadhaa mpaka mauti yalipomchukua jana.
Akiwa na kundi hilo, enzi za uhai wake marehemu Cool D na mwezake Kabago walifanikiwa kutoa albamu moja yenye jina la nawashangaa, iliyosimama kwa ngoma kama 'Bosi nipe mshahara wangu', 'Mwanza zirekebishwe barabara' na nyingine.
Blog hii inatoa pole kwa ndugu, jamaa na marafiki waliofikwa na msiba huo. Mungu aiweke roho ya marehemu mahali pema peponi. Amina
Monday, December 13, 2010
Posted in | |
1 Comments »
Bosi nipe mshahara wangu wimbo huu ntaupata wapi jamani nimetafuta mpaka nimechoka