Kutoka pande za Zenji, msanii Berry Black amesema na ebwanadaah kuwa, taarifa zilizorushwa na kituo kimoja cha redio ya burudani Bongo hivi karibuni kwamba aliburuzwa na promota mmoja aliyemvuta Uingereza kwa malipo kidogo hazina ukweli wowote.
Akipiga stori na blog hii leo kwa njia ya mtandao kutokea visiwani humo staa huyo wa ngoma ya 'Najua' alisema kuwa jamaa walimchana kwamba alipelekwa Uingereza kupiga shoo zaidi ya tano lakini mkwanja aliopewa na promota huyo siyo zaidi ya laki tatu kitu ambacho siyo cha kweli, bali alifanya shoo nne ambazo kila moja alivuta dola za Kimarekani zisizopungua 1500 (Msomaji unaweza kupiga hesabu kwa pesa ya Kibongo)
"Jamaa wanasema kuwa promota alinilainisha kwa maneno kwamba nitaenda kusafisha nyota kwasababu sijawahi kufika pande zile wakati mimi ninachoangalia ni maslahi ya kazi yangu, siyo kuuza sura au kusafisha nyota," alisema Berry.
Hivi sasa mchizi yuko Zenji kwa ajili ya mapumziko baada ya ziara hiyo ndefu, next week anatarajia kushuka kunako jiji la Dar kuendelea na mishe nyingie za kimuziki.
Read More......

Thursday, June 30, 2011
Posted in | |
0 Comments »