ILI MUZIKI WETU UWEZE KWENDA KIMATAIFA NI LAZIMA TUBADILIKE, SAPOTI YAKO PIA MUHIMU



Ishu iliyodondoka ndani ya Ebwanadaah hivi karibuni inahara kwamba, staa wa Bongo Muvi na muziki wa kizazi kipya, Hemed Suleiman na mshindi wa pili wa shindano la Tusker Project Fame mwaka jana, Peter Msechu wameitwa kwa ajili ya kujiunga na washiriki wengine katika muendelezo wa shoo hiyo itakayofanyika pande za Nairbi nchini Kenya.
Unajua nini kilichowafanya washikaji wapate zali kwa mara ya pili? Kwasababu mchongo mzima utakwenda kwa jina la Tusker Project Fame All Stars na unawahusu wale washiriki waliyowahi kufanya vizuri kwenye mashindano yaliyopita kama ilivyokuwa kwenye mpambano wa Big Brother mwaka jana.
Kitakachofuata baada ya washiriki wa Tusker kuanza kwenda hewani ni kura zitakazowawezesha kuibuka na ushindi. Jiandae.

Monday, June 6, 2011 Posted in | | 0 Comments »

One Responses to "HEMED, MSECHU WAITWA TUSKER PROJECT FAME ALL STARS"

Write a comment