ILI MUZIKI WETU UWEZE KWENDA KIMATAIFA NI LAZIMA TUBADILIKE, SAPOTI YAKO PIA MUHIMU

Kama nilivyokuahidi siku kadhaa zilizopita kwamba, nitavuta waya mpaka pande za Geita, Mkoani Mwanza na kucheki na msanii Godfrey Tumaini 'Dudubaya' ili aweke wazi kuhusiana na skendo yake ya kutupwa selo kama ilivyoripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari hivi karibuni.
Akipiga stori na ebwanadaah leo mchana Dudu amefunguka kwamba, ameshangazwa na baadhi ya vyombo vya habari kuripoti kuwa alitupwa selo na kulala ndani wakati ukweli ni kwamba alipofikishwa kituoni hapo alijidhamini na kuachiwa huru siku hiyo hiyo.
“Da! Nimeshangazwa sana na baadhi ya vyombo vya habari kama magazeti ya…..(anayataja) kwa kuandika kuwa nilikamatwa na kuswekwa lupango wilayani Geita ambamo nililala hadi asubuhi, ishu ambayo siyo kweli. Pia nimegundua kuwa waandishi wengine wa habari huwa hawawatendei haki wahusika kwasababu hakuna aliyenipigia na kuniuliza kilichotokea bali wao waliandika wanavyojua baada ya kusikia uvumi kwa watu ili mradi wanidhalilishe tu.
“Ni kweli nilikuwa nadaiwa shilingi 250,000 (laki mbili na nusu) na promoa mmoja huku Geita, ilikuwa ni kwa ajili ya kufanya shoo kwenye mkesha wa mwaka mpya yaani mwaka jana mwishoni lakini kutokana na sababu zilizokuwa nje ya uwezo wangu nilishindwa kutokea kwenye shoo yake. Hivi karibuni nilipoibuka pande hizi kwa ajili ya shoo jamaa akanitokea na polisi wakanikamata, tulipofika kituoni nikajidhamini kwa shilingi laki moja, siku iliyofuata yaani Mei 31 nikafikishwa mahakamani ambako nilishauriwa nilimlipe jamaa mkwanja wake ili tumalizane kwa amani.
“Nilikubaliana na hilo, tukapanga tumalizane mwezi huu tarehe 23 ambapo nitampa lakini moja na nusu iliyobaki. Ukweli ni kwamba hata kama ningekuwa sina pesa mfukoni nisingelala selo kwasababu huku Geita kuna kaka zangu wanafanya kazi mgodini, waliposikia niko polisi walikuja na balozi wa mtaa wao kwa ajili ya kunichukulia dhamana. Nimeshangazwa sana na stori za mimi kulala selo, nafikiria kitu cha kufanya ili tabia kama hii ya kudhalilishana kwenye vyombo vya habari bila sababu isijirudie tena kwa watu wengine”, alifunguka Dudu a.k.a Mamba.

Friday, June 10, 2011 Posted in | | 0 Comments »

One Responses to "DUDU AFUNGUKA KUHUSU KUTUPWA SELO"

Write a comment