Hii ni ngoma yangu mpya baada ya ile ya Hadithi, yaitwa 'Narudi Nyumbani', nimewashirikisha Cheleaman na Zuhura, kazi imefanyika Bamba Rec iliyopo Mbezi, Kibamba chini ya Producer Mobbaizoh aliyegonga ngoma ya Dongo Janja yenye jina la 'Anajua'. kazi hii tayari ipo katika baadhi ya vituo vya redio huku nikifanya maandalizi ya video yake. Nafahamu. Huu ni muendelezo wa kazi zangu za muziki mpaka kukamilisha albamu yenye jina la Historia ambayo itakuwa na nyimbo 8, bado kazi 3 ikamilike. Asante kwa sapoti yako mdau. Waweza kuisikiliza ngoma hapo juu kushoto.
Monday, June 6, 2011
Posted in | |
0 Comments »
One Responses to "HII NDIYO NGOMA YANGU MPYA"