Mratibu wa ishu hiyo, Edwin a.k.a Eddo wa Redio Ebony FM ya huko aliwataja wakali hao kuwa ni Fid Q, Matonya, Squezeer, Chegge, Madee, Tundaman, Blue, Baby Madaha, Linex, Nay wa Mitego, Dully, Felly na wengine kibao huku wale wapenzi wa mirindimo ya pwani wakirusha vidole juu na kundi la Coast Morden taarabu bila kuisahau bendi kali ya Sweat Noise ya Iringa.
"Pia kutakuwa na mchezo wa masumbwi kati ya mkali Rashid Matumla na 'Snake Boy' na Chupaki wa Iringa. Ishu zote hizo zitagongwa ndani ya Uwanja wa mpira wa Samora, Desemba 6, kuanzia saa sita mchana mpaka saa 12 jioni chini ya udhamni wa Kampuni ya simu za mkononi, Vodacom. Ni zaidi ya burudani," alisema Eddo. Read More......