Meneja wa Tip Top, Babu Tale
K-Sher (katikati) akiwa na baadhi ya wakali wa Tip Top
First Lady wa Kundi la Tip Top Connection lenye maskani yake pande za Manzese, Dar es Salaam, Khadija Shaban a.k.a K-Sher amesimamishwa kupiga mzigo ndani ya kundi hilo kwa kipindi kisichojulikana.
Akidondosha stori ndani ya ebwanadaah wikiendi iliyopita Meneja wa kundi hilo, Khamis Tale Tale a.k.a Babu Tale alisema kwamba wamefikia uamuzi huo baada ya K-Sher kuonesha utovu wa nidhamu kitu ambacho kimekuwa kikiwapa usumbufu kwa muda mrefu.
“Mara nyingi K-Sher amekuwa akifanya vitu ambavyo vinaleta usumbufu kwa wenzie, mfano hivi karibuni tulikuwa na shoo Mwanza, yeye alishindwa kufika kwa sababu tulishindwa kupata tiketi ya ndege kwa muda huo, wenzie walikuja kwa basi na kufanya shoo kisha kurudi Dar.
“Tulipofika Dar akawa anadai alipwe pesa za shoo hiyo, huku akitishia kujitoa kundini kama hatukufanya hivyo, siyo hilo tu yapo mengi ambayo msanii huyo amekuwa akiyafanya na kusababisha usumbufu kwa wenzie kitu ambacho kimetusukuma sisi viongozi kuchukua uamuzi wa kumsimamisha mpaka hapo baadaye,” alisema Tale.
Safu hii ilijaribu kumtafuta K-Sher kupitia simu yake ya mkononi ili naye aweke wazi kuhusu hilo lakini mpaka tunakwenda mitamboni hakuweza kupatikana. Tunaahidi tutaendelea kucheki naye, atakapopatikana kila kitu kitakuwa wazi kupitia gazeti la Ijumaa litokalo kila siku ya Ijumaa na hapa ebwanadaah.
Read More......
Sunday, August 29, 2010
Posted in | |
0 Comments »