ILI MUZIKI WETU UWEZE KWENDA KIMATAIFA NI LAZIMA TUBADILIKE, SAPOTI YAKO PIA MUHIMU


Sistaduu anayefanya vyema kwenye game ya muziki wa Kizazi Kipya, Zuhura Mrisho anadaiwa kuwa mgumu kinoma kung’oleka kimapenzi na maneno ya kitaa yanasema kwamba, ili umpate basi lazima upitie kwa sangoma kuweka mambo sawa kwanza.
Akipiga stori na ebwanadaah hii, Zuhura ambaye pia aliwahi kuiwakilisha Bongo kupitia Shindano la kumtafuta Kisura wa Afrika, Nokia Face Of Afrika 2006, alisema:
“Najaribu kuyaweka maisha yangu mbele kwanza, mambo mengine baadaye, sipendi mambo ya mapenzi, kwa sababu najua hayana future, napambana na life kwanza.”
Hata alipobanwa aeleze kwasasa yupo katika uhusiano na nani alitilia ngumu, akieleza kwamba hayo ni maisha yake binafsi na hapendi kuingiliwa ingawa msimamo wake ulibaki kuwa hana time kabisa na wanaume.
Pamoja na stori hiyo, hivi sasa Zuhura anasikika na mzigo mpya unaokwenda kwa jina la ‘Napagawa’ songi ambalo ndani yake lina mashairi ya kimapenzi, akiwa amepiga kolabo na Kindago wa TMK Majita.

Sunday, August 22, 2010 Posted in | | 0 Comments »

One Responses to "ZUHURA ASHUKA NA KALI YA MWAKA"

Write a comment