Hapa nikipiga naye stori
...akipozi kitandani
...akibeba mashine yake ya kazi
...hapa akiwa mzigoni, akipulizia rangi nyumba
Pozi lake
Kunzia leo ntakuwa nikiwaletea stori za maisha ya mastaa mbalimbali wa Bongo waliotembelewa na safu ya Mpaka Home Next Level inayopatikana ndani ya Gazeti la Risasi litokalo kila siku ya Jumatano. Kwa kuanza leo huyu hapa staa wa muziki wa Bongo Flava, fundi rangi na mjasiriamali Zuhura Mrisho Watuta.
Sinza Kumekucha, Dar es Salaam ndiyo anapofanya maishi yake, mengi kuhusu yeye cheki na intavyuu hapo chini.
Mpaka Home: Ndani ya mjengo huu ndiyo home au umepanga?
Zuhura: Hapa nimepanga, nyumbani kwetu labisa ni Mwanza maeneo ya Igoma.
Mpaka Home: Unamudu vipi gharama za kodi?
Zuhura: Kazi zangu kama kupulizia rangi, muziki na biashara za vitu mbalimbali zinanifanya nimudu gharama zote yakiwemo mahitaji yangu.
Mpaka Home: Unataka kutuambia huna mpenzi ambaye anakusapoti katika maisha yako?
Zuhura: Mpenzi yupo, lakini mahitaji yangu mengi huwa napambana mwenyewe.
Mpaka Home: Ukiwa na tatizo, nani wa kwanza kumkimbilia?
Zuhura: Huwa ni mama yangu mdogo ambaye anaishi maeneo ya Kariakoo kisha wanafuata ndugu zangu wengine.
Mpaka Home: Katika ishu zako zote, yaani kazi ya kupaka rangi, muziki, biashara na nyingine ipi inakuingiza mkwanja zaidi?
Zuhura: Hakuna zaidi ya kazi ya rangi, hata kama sijapata tenda sehemu huwa nakodisha mashine zangu na vifaa vingine vya ujenzi, jioni vinaleta hesabu.
Mpaka Home: Unapenda na kuchukia nini katika maisha yako?
Zuhura: Napenda maisha yenye furaha na amani, nachukia kunyanyasika.
Mpaka Home: Baadaye ungependa kuwa na familia ya watoto wangapi na umejiandaaje kwa hilo?
Zuhura: Ntafurahi zaidi nikifanikiwa kupata watoto wawili, nimejipanga na ninaendelea kujiandaa vyema ili baadaye watoto wangu waishi maisha mazuri.
Mpaka Home: Nini tofauti ya maisha yako ya zamani kabla hujawa maarufu na sasa?
Zuhura: Kwangu nadhani tofauti ni kujulikana tu, mambo mengine yako vile vile, huwa sina makuu.
Mpaka Home: Unauzungumziaje uchaguzi mkuu wa 2010 na sanaa yako ya muziki kwa ujumla?
Zuhura: Nawaasa Watanzania wachague viongozi watakaowaletea maendeleo ili baadaye wasije wakajuta. Kuhusu muziki hivi sasa nimeachia kazi mpya yenye jina la Napagawa, albamu inakuja
Mpaka Home: Tunashukuru kwa ushirikiano wako Zuhura.
Zuhura: Mi pia nashukuru, karibuni tena.
Wednesday, August 25, 2010
Posted in | |
0 Comments »
One Responses to "MPAKA HOME KWA ZUHURA"