ILI MUZIKI WETU UWEZE KWENDA KIMATAIFA NI LAZIMA TUBADILIKE, SAPOTI YAKO PIA MUHIMU

Safari yangu sana ilikuwa ni kwa njia ya reli ya kati, nikajitupa ndani ya train japo kuna sehemu nilibadili na kupanda mabasi
...nilipofika Tabora mjini ilibidi nipate mapumziko ya muda katika hospitali moja baada ya kuhisi uchovu wa nguvu
...hatimaye safari iliendelea
Nashukuru Mungu nilifika salama
Hapa ndiyo kitaani kwetu, maeneo ya Mpanda Hotel
Kwa wale waliyopitia katika shule hii ya sekondari ntakuwa nimewakumbusha mbali sana
Hili ndiyo jengo la Mahakama yetu ya mwanzo lililopo pande za Makanyagio

Nasikitika sikuwa hewani kwa takribani wiki tatu, hivyo basi ninayo kila sababu ya kuomba radhi kwenu hasa kwa wale wadau wa blog yenu hii ya ukweli, ebwanadaah. Sababu kubwa ilikuwa ni likizo ya kikazi ambayo ilinifanya nisafiri kwa ajili ya kwenda kuwajulia hali ndugu na jamaa huko nyumbani kwetu Mpanda, kwenye Mkoa mpya wa Katavi. Nashukuru Mungu nimerudi salama, mambo yetu yaani ishu za ukweli zitaendelea kudondoka pande hizi kama kawa. TUKO PAMOJA.

Sunday, August 22, 2010 Posted in | | 0 Comments »

One Responses to "HABARI ZETU WADAU, MKOA POA?"

Write a comment