ILI MUZIKI WETU UWEZE KWENDA KIMATAIFA NI LAZIMA TUBADILIKE, SAPOTI YAKO PIA MUHIMU

Ebwanadah wiki hii, ambayo inapatikana ndani ya gazeti la Ijumaa Wikienda kunako safu ya Abby Cool & MC George Over The Weekend inashuka kitaani na orodha ya mademu waliowahi kulala kitanda kimoja na dogo anayetesa katika muziki wa R&B pande za Marekani hivi sasa, Justin Bieber.
Kinda huyo raia wa Canada, akiwa ndiyo kwanza anagonga miaka 16 ya kuishi duniani tangu alipozaliwa mwaka 1994, tayari ameshakula bata na vimwana wawili, Caitlin Beadles kuanzia mwaka 2007-2008 kabla ya kufunga pazia na Kristen Rodeheaver mwaka 2009 huku maelezo yakisema kwamba, bado wapo pamoja hadi hii leo.
Wengi wa mashabiki wake waliotoa comments zao, walisema kwamba, dogo ni cheche sana na kama kwa umri huo tayari ameshamiliki vimwana wawili, basi akifikisha miaka ishirini huenda idadi ikawa kubwa zaidi.

Sunday, August 22, 2010 Posted in | | 0 Comments »

One Responses to "EBWANADAAH! WIKI HII"

Write a comment