Mkali wa Hip Hop Bongo, Kala Jeremah, ambaye ali-spend miezi kadhaa jijini Kampala Uganda akiwa na mchuchu aitwaye Jesca, amerejea nchini kimya kimya akiwa mikono mitupu, tofauti na matarajio ya wengi kuwa angekuja na mamsapu wake huyo.
Akiteta na ebwanadaah juzi, sosi wetu alisema: “Jamaa karejea, lakini yupo peke yake, wengi tuliamini angekuja na demu wake, lakini ndiyo hivyo, msela kashuka mwenyewe.”
Kala alipopigiwa simu ili kufafanua, alikuwa na haya ya kusema: “Yeah! Ni kweli sijaja na Jesca, lakini hiyo haimanaanishi kwamba tumeachana. She is still my love, nimeshindwa kuja naye kwa sababu uhusiano wetu haujawa plain kwa wazee wake, na mimi kama muungwana, sikuona busara kutoroka naye, ila kwa taarifa yako, ndoto yetu ni ndoa.”
Sunday, August 22, 2010
Posted in | |
0 Comments »
One Responses to "KALA ATUA BONGO BILA DEMU WA KIGANDA"