ILI MUZIKI WETU UWEZE KWENDA KIMATAIFA NI LAZIMA TUBADILIKE, SAPOTI YAKO PIA MUHIMU

Mkali wa ngoma za majonzi kutoka kruu ya Tip Top Connection, Khalid Ramadhani ‘Tundaman’ amesema na ShowBiz kwamba amepokea kwa mikono miwili pongezi anazopewa na baadhi ya mashabiki wake kuhusiana na ubora wa kazi zilizomo kwenye albamu yake mpya iitwayo ‘Hali yangu mbaya, inayosumbua sokoni kitaani hivi sasa, Hemed Kisanda anashuka nayo.
Akiangusha stori na safu hii juzi kati Tunda alisema kwamba amekuwa akipokea simu nyingi kutoka kwa mashabiki zinazompa ‘hala’ kwa utunzi bora wa nyimbo zake.
“Albamu ya Hali yangu mbaya ni elimu tosha kwa jamii kwa jinsi nyimbo zake zilivyokuwa na mafundisho ya kutosha, ndiyo maana napata pongezi. Pia katika albamu hiyo yenye nyimbo kumi kuna ngoma moja inakwenda kwa jina la ‘Uzuri wake’ ambayo nimemuimbia staa wa muvi Bongo, Rose Ndauka,” alisema.
Pia msanii huyo aliweka kweupe kwamba kwa wale wenye maswali kuhusu ndoa yake anatarajia kufanya hivyo mapema Februari mwaka ujao.

Friday, August 27, 2010 Posted in | | 0 Comments »

One Responses to "TUNDA AMPA SHAVU ROSE NDAUKA"

Write a comment