Mlezi wa Za Big Level, Aneth (kushoto) akiwa na Best Werema
Nikisalimiana na Best Werema, muasisi wa Za Big Level
...hapa nikisalimiana na Aneth
...zikafuatia picha za pozi
Leo mchana nilibahatika kutembelewa na memba wawili wanaounda familiy ya Za Big Level kutoka Tarime mkoani Mara, Best Werema ambaye ni muasisi wa umoja huo na Aneth Kubih 'First Lady' ambaye pia ni mlezi wa chama hilo ambao nilikuwa nikiwasiliana nao kupitia mtandao kwa muda mrefu bila kuonana hasa baada ya kuvutiwa na kazi zangu ukiwemo wimbo wangu mpya, Hadithi. Vijana hawa kwasasa wapo Dar kwa ajili ya kuangalia ni jinsi gani wanaweza kuusongesha zaidi umoja wao huo kwa kuongeza idadi ya wanachama ikiwezekana nchi nzima.
"Za Big Level ni family ambayo inawahusu vijana wengi hasa wenye vipaji tofauti kwa ajili ya kusaidiana na kuhakikisha kila mmoja anafanikiwa kupitia kipaji chake, ndiyo maana kauli mbiu yetu inasomeka kwamba, 'ZA BIG LEVEL KWA VIPAJI ZAIDI'. Kama wewe ni kijana na unahisi una kipaji chochote unakaribishwa kujiunga nasi," alisema Werema. Mengi zaidi kuhusu vijana hawa tembelea tovuti yao www.zabiglevel.blogspot.com.
Read More......
Sunday, January 30, 2011
Posted in | |
0 Comments »