ILI MUZIKI WETU UWEZE KWENDA KIMATAIFA NI LAZIMA TUBADILIKE, SAPOTI YAKO PIA MUHIMU

Mchizi aliyekuja vizuri katika sanaa ya muziki wa kizazi kipya, Godzilla jana alinusurika kufa baada ya kupigwa mzinga na ndinga alipokuwa kwenye Bajaj na mchizi wake wakielekea kunako studio za 24/7 zilizopo pande za mikocheni kwa Warioba.
"Tulikuwa kwenye Bajaj tukielekea studio ghafla tukashtukia tumepigwa kwa nyuma na gari, ajali ambayo ilisababisha nivunjike jino moja na majeraha mengine mdomoni, ila nashukuru Mungu hatukupoteza uhai. Hivi sasa tupo kituo cha polisi Oysterbay kwa maelezo zaidi," alisema Zilla ambaye kabla ya tukio hilo alikuwa akijiandaa kuutambulisha umoja wao, Zilla Inc.

Sunday, January 23, 2011 Posted in | | 0 Comments »

One Responses to "GODZILLA AVUNJIKA JINO AJALINI"

Write a comment