King katika pozi la kifalme
Ghetto King
King (kulia) na Producer Villy wa 24/7 Records
King (kulia) na Producer Athur wa Aegies Records
King studio
Kutoka pande za Kawe, Dar mchizi aliyeanza mishemishe za game ya muziki wa kizazi kipya kitambo, Saimon a.k.a Sai Dog au Ghetto King ameweka pezani plani zake kwa mwaka huu wa 2011.
Akisema na ebwanadaah, King alifunguka kwamba kwa kuanza tayari amedondosha video ya ngoma yake mpya yenye jina la Birthday ambayo imefuatiwa na audio yenye jina la Wanapagawa aliyowapa shavu Temba na Jos Mtambo wa Kigambonino ambayo imegongwa ndani ya studio za 24/7 chini ya prodyuza Villy.
"Wanapagawa itafuatiwa na video yake itakayoanza kufanyiwa kazi hivi karibuni kupitia Limire Production chini ya muongozaji Malcom. Kingine hivi sasa tunajipanga kuja na family itakayokuwa na vichwa vinne na madensa tisa wa ukweli ambayo tutaitambulisha hivi karibuni kila kitu kitakapokuwa tayari," alisema King ambaye jana alisheherekea siku yake ya kuzaliwa baada ya kutimiza miaka kadhaa duniani.
Sunday, January 23, 2011
Posted in | |
0 Comments »
One Responses to "GHETTO KING NA MIKAKATI YA 2011"