ILI MUZIKI WETU UWEZE KWENDA KIMATAIFA NI LAZIMA TUBADILIKE, SAPOTI YAKO PIA MUHIMU

Janja stejini
...hapa akiwa juu ya mkoko
..hapa akishangaa

Dogo anayekuja juu kukako game ya muziki wa kizazi kipya kutoka pande za A-Town, Abdul a.k.a Dogo Janja juzikati alijikuta katika wakati mgumu baada ya kuitungua bajaj kwa nyuma na kusababisha mtafaruku kwa saa kadhaa.
Ishu hiyo ilichukua nafasi maeneo ya Sinza, Dar wakati dogo alipokuwa akisukuma mkoko (gari) na kujikuta akiingia nyuma ya bajaj ambapo baada ya mzozo wa hapa na pale na raia waliyokuwa pande hizo askari polisi waliingilia kati na kuihamishia kesi hiyo kituoni.
Akipiga stori na ebwanadaah memba wa kundi la Tip Top Connection, Hamad Ally a.k.a Madee alisema kwamba, baada ya ishu hiyo kutinga mikononi mwa polisi waliingilia kati na kuimaliza kiutu uzima. "Unajua dogo haruhusiwi kuendesha gari barabarani zaidi ya kule kwetu uchochoroni lakini aling'ang'ania aachiwe na mchizi wetu aliyekuwa naye wakielekea Tip Top.
Ndiyo maana tukaiwahi ishu hiyo kabla haijafika mbali. Kosa hilo halitajirudia tena, tutamuweka chini na kumpa darasa kuwa umri wake haumruhusu kuendesha gari".

Sunday, January 23, 2011 Posted in | | 0 Comments »

One Responses to "DOGO JANJA AITUNGUA BAJAJ"

Write a comment