ILI MUZIKI WETU UWEZE KWENDA KIMATAIFA NI LAZIMA TUBADILIKE, SAPOTI YAKO PIA MUHIMU

Q Jay

<!--[if gte mso 9]> Normal 0 false false false EN-US X-NONE X-NONE MicrosoftInternetExplorer4
Siku chache baada ya msanii wa muziki wa kizazi kipya, Joseph Mapunda ‘Q Jay’ kutangaza kuokoka na kuachana na muziki wa kidunia ameifanya idadi ya wasanii wa muziki huo waliomrudia mungu kuongezeka.

Kwa mujibu wa uchunguzi uliyofanywa na ebwanadaah, Q Jay anaifanya idadi ya wasanii wa muziki wa kizazi kipya waliyomrudia Mungu wao kufikia zaidi ya watano akiwemo Zedawi aliyekua katika kundi lao, Wakali Kwanza.

Pia wasanii kama Renee Ramila, K-Basil, Spuller na wengine pia waliachana na muziki wa kizazi kipya na kurudi kundini. Kwa upande wa Nuruel aliwahi kutangaza kuachana na muziki wake na kuingia wenye nyimbo za Injili lakini baadaye alitoka huko na kurudi tena kwenye Bongo Flava bila kuweka wazi sababu hasa iliyomrudisha.

Wednesday, April 20, 2011 Posted in | | 0 Comments »

One Responses to "Q JAY AWAFUATA KINA K-BASIL KWENYE WOKOVU"

Write a comment