ILI MUZIKI WETU UWEZE KWENDA KIMATAIFA NI LAZIMA TUBADILIKE, SAPOTI YAKO PIA MUHIMU

Kutoka ndani ya mradi wa muziki wa kizazi kipya, mchizi kutoka pande za Manzese, Dar es Salaam, Emanuel Elibariki a.k.a Ney wa Mitego ambaye yuko hewani na ngoma yake mpya, 'Itafahamika' ambayo ndani imewachana laivu baadhi ya mastaa wa Bongo Flava, wiki iliyopita chupuchupu azichape na washikaji ambao hawakufahamika mara moja ni akina nani.

"Ilikuwa pande za Mwenge, nilikuwa nimesimama maeneo fulani mara washikaji wawili wakaniibukia na kuanza kunipiga maswali mawili matatu huku wakihoji kwanini nimewachana watu kwenye wimbo wangu, mara wakaanza kunisogelea na kunishika shati, bahati nzuri pembeni kulikuwa na wanangu ambao walipoona mchezo huo waliingilia kati na kuwafanya jamaa waachane na mimi na kuondoka huku wakipiga mkwara kwamba lazima wanifanyie umafia," alisema mchizi.

Read More......
Monday, August 31, 2009 Posted in | | 0 Comments »


Kutoka ndani ya familia ya TMK Family, ishu mpya iliyodondoka ndani ya ebwanadaah hivi punde inasema kwamba, baada ya kusumbua na ngoma yake, 'Maneno nawafunza' msanii Amani James a.k.a Temba, Drakula au Mbabe wa mdomo siku chache zijazo atadondosha ngoma mpya yenye jina la Muda unaruhusu aliyompa shavu mwanadada Enika.
"Ngoma imefanyika Bongo Records kwa Majani, ni mapinduzi mengine katika game ya muziki wetu wa kizazi kipya," hiyo ni kauli ya Temba.

Read More......
Friday, August 28, 2009 Posted in | | 0 Comments »


Madee
Babu Tale

Inawezekana ishu kubwa iliyopo kunako game ya muziki wa kizazi kipya hivi sasa ni kuendelea kubomoka kwa Kundi la Tip Top Connection, kitu ambacho kimewafanya baadhi ya wadau wa burudani Bongo watutumie meseji nyingi wakitaka kufahamu mdudu gani hasa ambaye anatishia amani ndani ya umoja huo.
Kwa kumbukumbu za ShowBiz, alianza kuchomoka MB Dog huku mkononi akiwa na faili la sababu ikiwemo kuambulia mkwaja kiduchu kwenye mauzo ya albamu yake, akafuatiwa na Deso aliyekuwa akipiga kazi sambamba na Pingu ambaye pia aliitaja sababu kubwa ni kuambulia ankara za kitoto kwenye mauzo ya kazi yao.
Kabla watu hawajasahau, mwezi uliyopita ÔdogoÕ Z-Anto naye alichomoka na kudai kwamba mkataba wake na familia hiyo umeisha hivyo ameamua kugeukia upande mwingine kwa kupiga kazi chini ya uongozi mpya ambao hajautaja hadi hii leo. Vile vile msanii Pingu ambaye alisimama vyema kwenye kolabo ya ngoma ya ÔBinti KiziwiÕ naye ameonesha nia ya kusepa kwani tangu alipochomoka Z-Anto hajawahi kutokea kunako maskani ya umoja huo wala kuambatana kwenye shoo yoyote ya Tip Top.
Hivi juzi msanii Spark aliyesimama vyema kwenye ngoma ya Nipe Ripoti na Tunda aliendelea kuipunguza kasi ngome hiyo kwa kuachia ngazi huku akiwa na sababu kibao, zikiwemo kutofaidika na umoja huo na kwamba ameamua kupiga kazi kivyake kwakuwa uongozi wa Tip Top haukua fea kwa upande wake na anachohangaikia kwa sasa ni safari yake ya muziki baada ya kujitoa kundini humo.
ShowBiz kama mdau namba moja wa burudani za Kibongo, hususan game ya muziki wa kizazi kipya iliamua kuingia mtaani ili kupata ukweli wa yote hayo na nini chanzo za wasanii hao kuendelea kujiengua Tip Top. Kwa kuanza ilipiga stori na msanii Hamad Ally a.k.a Madee ambaye ni memba namba moja wa familia hiyo ili kujua anauzungumziaje mmomonyoko huo.
ÒMimi kama muasisi wa Tip Top Connection ambaye niliitoa Manzese na kuipeleka pande za Kagera wanapoishi viongozi wetu Abdul Bonge na Babu Tale bado sijajua kwanini wasanii hao wanaojitoa, hawataki kunishirikisha mimi kwakuwa wanapokuja mtu wa kwanza kukutana naye ni mimi ambapo baada ya kuwasikiliza nawapeleka kwa uongozi kabla ya kukubaliwa na kufanya kazi.
ÒKwa mfano MB Dog siku ya kwanza kabisa alikuja na Cheleaman nikawasikiliza, baada ya kuona wako fiti nikawapeleka kwa kina Bonge japo baadaye Chelea alijitoa akabaki Dog peke yake ambaye alikuja pale hana kitu lakini alisikika na kuwa na mafanikio, cha ajabu wakati anaamua kujitoa hakutaka hata kuniambia, nikamsikia kupitia vyombo vya habari tu.
ÒVile vile kwa Pingu na Deso ilikuwa hivyo hivyo japo wao hawakupata mafanikio makubwa sana kutokana na albamu yao kufanya vibaya sokoni, lakini walimudu maisha ya kujitegemea kupitia Tip Top. Ukiachia mbali na hao, msanii kama Z-Anto kafanyiwa vitu vingi sana na Tip Top lakini mwisho wa siku hakutaka hata kuniomba ushauri mimi kabla ya kutoka.
ÒKwa upande wa Spark ndiyo usiseme, alikuja pale kupitia mimi nikampeleka kwa Abdul Bonge japokuwa alionesha kumkataa, nikiwa na Babu Tale (Meneja msaidizi) tuimsimamia mpaka akafanikiwa kuwa juu kupitia umoja wetu, lakini nashangaa leo hii anajitoa bila kutaka ushauri wangu mimi kama msanii mwenzake zaidi ya kuulaumu uongozi.
ÒKuhusu hayo yote mimi kama mwana Tip Top halisi napenda kuwashauri wasanii waliopo na waliojitoa kundini kwamba, wasipende kutumia njia hiyo ili kujitangza zaidi kwani kuna wengine huwa wanatoka na kurudi, muziki ni maisha yao wanachotakiwa kufanya ni kuangalia ni kitu gani hasa wanakipata katika sanaa hii, siyo baada ya miaka kadhaa inabaki historia tu kuwa fulani zamani alikuwa msanii bila kuwa na aset yoyote,Ó alisema Madee.
Kwa upande wake meneja msaidizi wa kundi hilo, Babu Tale ambaye ndiye amekuwa akilalamikiwa zaidi alisema kwamba hahitaji kuwazunguzia sana wasanii waliojitoa bali amegundua kwamba kufanya kazi kiushikaji bila kuwa na mikataba ya kueleweka ni tatizo, kitakachofuata hivi sasa ni kujipanga upya kwani anaamini Tip Top haitakufa kwa sababu ya wasanii waliotoka.
ÒUnajua mimi ningeandikishiana mkataba na msanii kama Tunda ningemfunga tu, kwakuwa asingweza kuufuata ndiyo maana nikaamua tufanye kazi kiushikaji, lakini madhara yake tumeyaona na tayari tumejifunza kitu. Siyo kwamba najisikia vibaya wasanii wakijitoa isipokuwa inanikera zaidi pale wanapokwenda kunizungumzia vibaya wakati nimewafanyia mambo mengi ambayo hawakutarajia. Zaidi nawatakia mafanikio mema katika safari ya muziki wao,Ó alisema Babu Tale ambaye pia alimuwakilisha Abdul Bonge.
Je, wewe mdau wa burudani una lolote kuhusiana na ishu hii, tuambie kwa meseji 0715-110 173 ili tuwarushie wahusika.

Read More......
Posted in | | 0 Comments »



"Napenda kuwa na mke mwenye heshima na adabu wakati wote na asie na ubaguzi hata kidogo na mwenye kuendana nami"

Kijana toka pande za Sinza ambaye anapiga kazi ndani ya kundi la TMK Wanaume Family, Saidi Juma Hassan a.k.a Chegge Chigunda, Mtoto wa Mama Said ndiye staa aliyetiliwa maguu na Mpaka Home na kuangusha naye stori kibao kuhusiana na maisha yake hasa nje ya muziki.
Kama tulivyomtambulisha hapo juu, Sinza Madukani, Dar es Salaam ndiyo sehemu anayofanya maisha yake. Majira ya mchana, wiki iliyopita Mpaka Home ilikuwa kwa mchizi ambaye amepanga kunako gheto moja la kiushikaji. Shuka chini ili ujue mengi zaidi kuhusu maisha yake.
Mpaka Home: Inakuwaje Chegge, siku zote nilikuwa nadhani unaishi Temeke, lini umehamia Sinza?
Chegge: (Kicheko kidogo) mimi miaka yote ya maisha yangu huwa naishi Sinza, hata familia yangu karibu yote ipo jirani tu kutoka hapa.
Mpaka Home: Je, unaishi vipi na majirani zako?
Chegge: Niko nao vizuri sana, tena wananipenda ile kichizi mtu wangu, sijawahi kusikia tuhuma hata moja ya kuniponda kutoka kwa majirani zangu hata machizi wangu wote wa kitaa.
Mpaka Home: Kitu gani usichokipenda katika maisha yako?
Chegge: Nawachukia sana watu wanaopenda kukwamisha maendeleo yangu na wezi wa kazi zetu kwa ujumla.
Mpaka Home: Unadhani lini utakuwa na mjengo wako na kuepukana na adha ya kupanga?
Chegge: Siku yoyote, hiyo mipango ipo naamini Mungu ndiye mpaji.
Mpaka Home: Unalionaje shindano lako la kutafuta mke linaloendelea katika gazeti hili?
Chegge: Nadhani litanisaidia kwa kuwa matarajio yangu baadaye ni kuwa na mke na ningependa Mpaka Home iwe ya kwanza kulijua jambo hilo.
Mpaka Home: Ungependa kuwa na mke mwenye tabia zipi?
Chegge: Napenda mwanamke yoyote mwenye heshima na adabu wakati wote na asiye na ubaguzi hata kidogo na mwenye kuendana nami.
Mpaka Home: Mpangilio mzima na ratiba yako kwa siku umekaaje?
Chegge: Mara nyingi ninapokuwa bize na mazoezi ya kundi huwa naamka saa nne asubuhi, ninaporudi home nahitaji muda mwingi wa kukaa na kuandika nyimbo mpya, baadae najipunzisha.
Mpaka Home: Kwenye suala zima la kujiachia yaani kwenda katika sehemu mbalimbali za starehe kwako limekaaje?
Chegge: Hilo lipo, siku moja moja huwa machizi wangu wa kitaa wananipitia tunaenda kujichanganya maeneo mbalimbali.
Mpaka Home: Huwa unapenda kuandika mashairi wakati gani, ikiwemo kuingiza sauti studio?
Chegge: Mara nyingi huwa inategemea na mudi, kama ipo muda huo huo naandika, kuhusu kuingiza sauti (kurekodi) huwa inategemea na ratiba za studio.
Mpaka Home: Hivi sasa ukipata tatizo nani wa kwanza kumkimbilia?
Chegge: Mtu wa kwanza ni mama yangu mzazi kwa kuwa ndiye yuko karibu sana na mimi.
Mpaka Home: Unapendelea msosi wa aina gani?
Chegge: Kwenye suala la misosi huwa sichagui, wowote unaokubali kuingia kinywani huwa nakandamiza tu.
Mpaka Home: Unanufaika vipi na muziki wako hasa ukiwa kwenye kundi?
Chegge: Nanufaika na mambo mengi sana nikiwa ndani ya kundi ikiwemo kupata shoo nyingi ambazo naamini nikiwa peke yangu ni vigumu kuzipata.
Mpaka Home: Nini kauli yako kwa mashabiki wako na jamii nzima kwa ujumla?
Chegge: Wote kwa ujumla wakae mkao wa kula kusikiliza mipini yangu mipya ambayo itakuwa ndani ya albamu yangu ya tatu itakayokwenda kwa jina la ÔKaribu kiumeniÕ. Hivi karibuni nitaachia ngoma nyingine mpya itakayokwenda kwa jina la Mambo Bado ambayo nimemshirikisha Lady Jaydee.
Mpaka Home: Poa Chegge, pamoja sana.
Chegge: Nashukuru, karibu tena.

Read More......
Posted in | | 0 Comments »

Kutoka kiwanja leo tunashuka na uhusiano 10 wa kimapenzi wa mastaa mbalimbali ambao ndani ya mwaka huu ulisambaratika kutokana na kuhitilafiana kwasababu kadhaa japokuwa kuna baadhi yao inasemekana wamerudiana hivi karibuni.
50 CENT na Ciara
Mwana Hip Hop, 50 Cent wa Marekani aliripotiwa kuachana na aliyekuwa mchumba wake, Ciara Harrison. Rafiki wa karibu na Ciara aliueleza mtandao mmoja kuwa, mwanadada huyo aliachia uamuzi huo baada ya kugundua kwamba 50 Cent alikuwa hajatulia.
Usher na Tameka
Usher Raymond na Tameka Foster ambao walifunga ndoa ya nguvu na kufanikiwa kupata watoto wawili, siku kadhaa zilizopita waliripotiwa na vyombo mbalimbali vya habari kuachana, kabla ya wao kuweka wazi hadharani.
Licha ya uhusiano huo kuvunjika tangu mwaka jana, Tameka anayeishi Las Vegas hivi karibuni aliiambia Mahakama ya Fulton kuwa, bado anautambua uhusiano wao uliyofikia tamati Juni 6 mwaka huu.
Jon na Kate Gosselin
Muigizaji Kate Gosselin amesema kuwa, alitengana na mumewe tangu miaka miwili iliyopita.
Msanii huyo ambaye ndoa yao ilidumu kwa miaka 10, alikubali kuishi katika maisha ya upweke.
Paris Hilton & Doug Reinhardt Split
Mwanamitindo, Paris Hilton naye amekuwa ni miongoni mwa mastaa waliyokutana na dhahama hiyo mara kibao kwani hivi karibuni alipigana chini na mpenzi wake, Doug Reinhardt.
Kanye West na Amber Rose.
Mwana Hip Hop, Kanye West mara kadhaa naye amekuwa akiripotiwa kuachana na kipenzi chake, Amber Rose.
CAmeron Diaz na Paul Sculfor
Mastaa wengine waliyotajwa kutosana mwaka huu ni Cameron Diaz na Paul Sculfor, ambapo jarida la Uingereza, Grazia limenukuu chanzo kimoja cha wawili hao kumwagana kuwa ni mawasiliano hafifu waliyokuwa nayo.
Jermaine Dupri
Baada ya kudumu kwa muda wa miaka saba, hivi karibuni Janet Jackson na mpenzi wake, Jermaine Dupri wameripotiwa kuachana.
Mastaa wengine ni Britney Spears aliyeachana na Jason Trawick, Joe Jonas naye ameripotiwa kuachana na Camilla Belle. Kwa upande mwingine mwanamuziki Jessica Simpson na Tony Romo uhusiano wao umefikia tamati mapema mwezi huu ikiwa ni siku chache baada ya aliyekuwa mume wake, Jessca, Nick Lachey kuachana pia na mchumba wake, Vanessa Minnillo.

Read More......
Posted in | | 0 Comments »

KULA FEGI DOGO, SIUNAJUA SAFARI NDIYO KWANZA INAANZA. Wasanii Kassim wa Tip Top na Berry Black kutoka pande za Zenji walipokuwa safarini hivi karibuni kunako ziara ya makundi mawili yaliyoungana, Tip Top Cennection na TMK Wanaume Family.

Read More......
Sunday, August 23, 2009 Posted in | | 0 Comments »

Kutoka pande za A-Town, mchizi aliyesumbua na ngoma yenye jina la 'Staili 3', Jarome Frank a.k.a Stopa Rhymes ameamua kuja kivingine na ngoma yenye jina la 'Na hustle' ili kuwaonesha fans wake kwamba kila staili anaweza kugonga.


Akipiga stori na ebwana daah, Stop alisema kwamba, katika kazi hiyo amesimama na mzee wa kulalamika 'Rama D' na kwamba huo ni utambulisho wa albamu yake ya pili inayotarajiwa kuanguka kitaani hivi karibuni.

"Albamu yangu ya kwanza iliitwa 'Shule ya Bure' na ilikuwa na ngoma kama 'Jiwe' niliyomshirikisha Nature, Staili tatu niliyosimama mwenyewe na nyingine za ukweli," alisema mchizi.

Read More......
Posted in | | 0 Comments »



'Ze big tolu' Hasheem Thabeet aliyekula dili Marekani kupitia game ya mpira wa kikapu akijifua pamoja na washikaji katika uwanja wa mchezo huo uliyopo pande za Chuo Kikuu, Dar es Salaam. Jamaa anatarajia kuondoka hivi karibuni kwenda kuendelea na ajira yake huko kwa Mzee mzima Obama

Read More......
Posted in | | 0 Comments »


"Usiombe uchawi wa mzungu (video kamera) uwe mbele yako halafu uambiwe ongea, hasa kujibu maswali. Lakini m2mzima nilimudu, siunaona"
Wiki hii warembo wanaowania taji la Miss Kiswahili, walidondoka pande za ofisini kwetu wakiongozwa na timu ya wafanyakazi wa kituo cha televisheni cha c2c ili kujionea maujanja tunayotumia katika kuandaa magazeti yetu. Mimi pia nilipata chansi ya kupoga nao stori na kujibu maswali niliyoulizwa na warembo hao kupitia kwa mtangazaji, Anti Lulu anayefanya vyema katika vipindi kama DK 5, Nyumbani ni Nyumbani na vingine vya TV hiyo ya kijanja.

Read More......
Friday, August 21, 2009 Posted in | | 0 Comments »

Tunda na Spark enzi za ushikaji wao
Ebwana daah! Ishu mpya iliyonifikia hivi juzi inasema kwamba, baada ya msanii Spark kujitoa ndani ya umoja wa Tip Top Connection, msanii Tundaman aliyegonga naye ngoma ya Nipe ripoti amemtaka swahiba wake huyo aache mara moja kuitumia kazi hiyo kwa kuwa ni mali yake.

TUNDA: Yeye kama ameamua kujitoa Tip Top, inabidi aachane na ngoma hiyo, kwakuwa mimi ndiye mtunzi, nilimpa shavu tu ili kumuweka juu kwakuwa kipindi hicho hakuwa akisikika. Hiyo ishu ya kujitoa inatufanya sisi wasanii wa familia hiyo tuonekane hatuna msimamo.

SPARK: Kweli yeye ndiye alikuja na idea ya wimbo huo lakini bila mimi, ngoma ya Nipe Ripoti isingekuwa vile. Mimi ndiye niliyeandika vesi yangu pamoja na korasi ambayo niliifanyia studio kwa MJ, shahidi wangu Marco Chali. Au kama Tunda anabisha uwekwe mpambano wa kuimba ngoma hiyo ili tuona nani atapotezwa. Mimi nimejitoa Tip Top kwa maslahi yangu, yeye pia inabidi ajizungumzie yeye na siyo kunitaja mimi kwenye intavyuu anazofanya.

Read More......
Posted in | | 0 Comments »

Mombasa raha bwana; mkubwa Fella na wanawe sambamba na Abdul Bonge wa Tip Top
Dully, Kassim na Abdul Bonge
Safari hii Dully pia aliongeza nguvu
Kitu cha 'Awena' (Kassim)
Madee akisem na fans wake
'Yes yes no bifu, Wanaume kazini'

Baada ya kuangusha shoo kadhaa zenye mafanikio katika pande mbalimbalo Bongo, muungano wa makundi mawili, TMK Wanaume Family na Tip Top Connection hivi majuzi ulidondoka pande za Mombasa nchini Kenya na kufanya kile kilichowapeleka, huku mashabiki kibao wakishangweka nao.

Read More......
Posted in | | 0 Comments »


Komedian aliyekwenda eji Bongo, Rashid Mwinshehe A.K.A Kingwendu ameingizwa mjini na promota mmoja anayekwenda kwa jina la Jumanne Mabawa a.k.a Baba D Askofu wa jijini Mwanza.
Kingwendu alisema na ebwanadaah mapema wiki hii kwamba, promota huyo amemtia ndani kiasi cha fedha shilingi milioni 1.5 ambazo aliziingiza baada ya kupiga mzigo Kanda ya Ziwa kupitia shoo zaidi ya kumi alizofanya kwenye visuwa vilivyopo Sengerema.

"Jamaa amenifanyia kitu kibaya sana, alinichukua vizuri Bongo akanipa advance, kula, kulala haikuwa na matatizo, kwahiyo nikamuamini lakini kumbe siyo mtu kihivyo.

'Baada ya kupiga shoo kwenye vijiji vya Zalagula, Kasaratu, Nyanango na Kanyala jijini Mwanza, nilikuwa nimekusanya shilingi milioni 1.5 kibindoni lakini juu kwa juu nilipata 'dili' kwahiyo nikaunganisha shoo. Lakini kabl sijaenda kupiga kimeo hicho pabde hizo hizo promota wangu aliniomba nimpe pesa hizo ili akaniwekee kwenye akaunti yangu kwakuwa maeneo ya huko yalikuwa siyo poa kutokana na wimbo wa majambazo lililoshamiri.

Kwa sababu nilikuwa nimeshamuamini nilimpa mkwanja hyo lakini huwezi kuamini, baada ya kurudi Dar na kwenda kuchungulia benki nikabaki hoi (hakukua na kitu) na kila nikimpigia simu ni stori tu. Hivi sasa nimemfungulia mashataka polisi kwa kosa la wizi wa kuaminiwa".

Read More......
Posted in | | 0 Comments »


Hii ni miongoni mwa kazi nazofanya kwa ajili ya kukupa wewe burudani na kujua ishu mpya kutoka kwa mastaa wetu wa Kibongo

Read More......
Posted in | | 0 Comments »

"Nazimia zaidi kitu cha wali kwa maharage"

Mpaka Home ambayo inapatikana ndani ya Gazeti la Risasi kila siku ya J'5 bado iko na wewe msomaji, ishu kubwa ikiwa ni kukuletea full stori kuhusu maisha ya mastaa wetu wa Kibongo. Je, unafahamu Tundaman kutoka ndani ya familia ya Tip Top Connection anaishije?
Swali hilo ndilo lililotufanya sisi kudondoka pande za Ubungo Maziwa, Dar es Salaam anakoishi mchizi na kupiga naye stori za kutosha kuhusiana na laifu yake kwa ujumla. majira ya saa 5:30 asubuhi, mwishoni mwa wiki iliyopita Mpaka Home ilkuwa tayari imesharipoti maeneo hayo.
Kama haulifahamu jina lake kamili, anaitwa Khalid Ramadhani Tunda, nyumbani hapo anaishi peke yake kama mpangaji ambaye ametokea kuelewana sana na baba mwenye nyumba wake. Aliipokea Mpaka Home kama mfalme na kutoa ushirikiano wa kutosha. Ishu nyingine kuhusu yeye shuka kwenye intavyuu ya ukweli hapo chini.
Mpaka Home: Niambie Tunda. Naona kama hauko poa, ndiyo unaamka?
Tunda: Poa. Nimeamka muda mrefu nilikuwa napiga tizo, si unaona mwili wa mazoezi huu.
Mpaka Home: Kabla hujahamia pande hizi za Ubungo ulikuwa unaishi wapi?
Tunda: Nilikuwa naishi home maeneo ya manzese Argentina.
Mpaka Home: Una muda gani tangu uhamie hapa?
Tunda: Miezi tisa au kumi.
Mpaka Home: Unaishi vipi na majirani zako hapa?
Tunda: Naishi nao poa, tena kwa ushirikiano mwema.
Mpaka Home: Unachukia kitu gani katika maisha yako? Tunda: Nachukia sana majungu, na umbea.
Mpaka Home: Kitu gani kigumu zaidi kwenye laifu yako?
Tunda: Kigumu zaidi ni kutafuta pesa.
Mpaka Home: Naona unaishi kisela, unatarajia kuoa lini?
Tunda: Mungu akipenda mwakani, itakuwa sambamba na ya Berry Black wa Zanzibar.
Mpaka Home: Kwanini unataka kuoa siku moja na Berry Black?
Tunda: Tumepanga kufanya hivyo kwakuwa pia tunatarajia kutambulisha albamu zetu kwa pamoja baada ya kuoa.
Mpaka Home: Unapenda kuwa na mke wa aina gani?
Tunda: Mwenye kujiheshimu, mkarimu na mzuri wa asili.
Mpaka Home: Ratiba yako kila siku ikoje?
Tunda: Mara nyingi inategemea na siku yenyewe. Kuna siku huwa naenda kwenye mazoezi ya mpira wa miguu asubuhi, baadaye mchana naafanya mazoezi ya muziki ndani ya studio yangu nyumbani.
Mpaka Home: Ukipatwa na tatizo nani wa kwanza kumkimbilia?
Tunda: Mama yangu mzazi, kwa kuwa ananipenda kuliko watu wote duniani, mi pia nampenda.
Mpaka Home: Unapendelea msosi gani zaidi?
Tunda: Wali maharage.
Mpaka Home: Historia yako kwa kifupi ikoje?
Mpaka Home: Nini matarajio yako kwa sasa kimuziki?
Tunda: Hivi sasa nawaandalia mashabiki wangu albumu mpya yenye jina la 'Kapteni wa Bongo Flava' ambayo Desemba mwaka huu itakuwa tayari.
Tunda: Mimi ni mtoto wa pili kati ya wanne tuliyozaliwa kwa mama yetu, kwa upande wa baba ni mtoto wa saba kati ya kumi na mbili. Nimesoma shule ya Msingi Makurumla iliyopo Magomeni Mwembe Chai, Dar es Salaam kuanzia 1993 hadi 2000. Hivi shule hiyo inaitwa Nyerere. Nilijiunga shule ya Sekondary ya Forodhani, Dar es Salaam 2001-2005. Katika game ya muziki mwanzo nilikuwa mtunzi wa nyimbo na kuwauzia wasanii, nikaona hilo halina maslahi nikaamua kuimba mwenyewe kwa kuwa nina kipaji.
Mpaka Home: Asante sana Tunda.
Tunda : Nami nashukuru pia kwa kunitembelea.

Read More......
Posted in | | 0 Comments »

Kwa ishu za kijanja kuhusu burudani za Kibongo na nje, cheki safu hii kwenye Gazeti la Ijumaa Wikienda kila siku ya J'3. Hii ndiyo ipo mtaani sasa. Pamoko sana

Read More......
Sunday, August 16, 2009 Posted in | | 0 Comments »

Read More......
Friday, August 14, 2009 Posted in | | 0 Comments »

Ule mpambano wa nguvu unaoendeshwa na Gazeti la Ijumaa kila mwaka kupitia safu ya ShowBiz umeanza rasmi wiki hii. Unachotakiwa kufanya ni kumpigia kura staa ambaye unadhani ana mvuto wa kuwa Ijumaa Sexiest Barchelor. Usikose kuicheki safu hiyo wiki ijayo ili kujua kinachoendelea.





Read More......
Posted in | | 0 Comments »

TMK, Tip Top Kazini
Cheki shazi


Madee akisema na watu wake wa pande hizo
Berry Black nae alitoa sapoti ya ukweli
B Dazan, Ncha Kali na ???? pia walikuwepo
Jirani pia aliniwakilisha. Hapa akiteta na Dj Fetty wa Clouds FM
Mchomvu: Mi pia nipo pande hizi
Viongozi wa msafara huo; Abdul Bonge (kushoto) na Mkubwa Fella

Read More......
Tuesday, August 11, 2009 Posted in | | 0 Comments »


"Hivi sasa sina mpenzi, bado nipo nipo sana"

Hii hapa ni Mpaka Home nyingine ya ukweli ambayo itakudondoshea maisha halisi ya msanii Baby Madaha ambaye kimuziki alifahamika kupitia shindano la Bongo Star Search (BSS) 2008, akaendelea kujituma hadi leo hii ambapo ana albamu moja yenye jina la ÔAmoreÕ, akiwa chini ya Kampuni ya Pilipili Entertainment.
Kimaisha binti huyo mrembo kapiga kambi pande za Kinondoni kwa Manyanya, Dar es Salaam akiwa ni mpangaji kunako bonge la nyumba. Ili kujua mengi kuhusu yeye shuka chini ucheki bonge la intavyuu.
Mpaka Home: Inakuwaje Baby, uko mzuka. Ndani ya mjengo huu wa kisasa unaishi na nani?
Madaha: Mimi niko poa. Hapa naishi peke yangu.
Mpaka Home: Ni jitihada zako mwenyewe au kuna mtu anakupa shavu kimtindo?
Madaha: Hakuna mtu yeyote anayenipa shavu zaidi ya Kampuni ya Pilipili ambayo nafanya nayo kazi.
Mpaka Home: Ratiba yako siku zote ikoje?
Madaha: Mara nyingi huwa nawahi sana kuamka, kitu cha kwanza kufanya huwa ni mazoezi ya kukimbia, natoka hapa mpaka beach. Nikirudi naingia bafuni kuoga kisha natafuta kinywaji baridi kama soda au juisi.
Mpaka Home: Kwanini iwe juisi na sio chai?
Madaha: Chai huwa sipendelei kabisa, yaani imenikalia kushoto.
Mpaka Home: Nini unapenda zaidi kufanya unapokuwa nyumbani?
Madaha: Kusikiliza nyimbo zangu na kufanya kazi kwenye kompyuta.
Mpaka Home: Vipi katika mambo ya maakuli, unaingia jikoni au ndio usupa staa?
Madaha: Hata hivi sasa tunapoongea nimebandika nyama jikoni.
Mpaka Home: Unapendelea zaidi kupika msosi gani?
Madaha: Wali, nyama na mbogamboga.
Mpaka Home: Vipi kuhusu kujipodoa, unamaindi?
Madaha: Yaani mimi ndio mama wa mamekapu.
Mpaka Home: Unapendelea mavazi ya aina gani?
Madaha: Napenda shoti pensi, top na jinsi.
Mpaka Home: Nini kiliwahi kukuumiza sana maishani mwako, nini kilichokufurahisha zaidi?
Madaha: Niliumia sana nilipofiwa na baba yangu mzazi, na nilifurahi sana nilipofanikiwa kutoa albamu yangu ya kwanza ya Amore
Mpaka Home: Kitu gani ambacho ni kero kubwa kwako?
Madaha: Majungu ndiyo kero kubwa kwangu.
Mpaka Home: Vipi kuhusu mpenzi, unaye?
Madaha: Hapana, hivi sasa bado nipo nipo sana tu.
Mpaka Home: Nakushukuru sana Baby.
Madaha: Asante sana, karibu tena.

Read More......
Posted in | | 0 Comments »

Akipaki
Humu ndiyo mwanangu Tunda anamojifariji baada ya kazi ngumu
Wakati Tunda akininong'oneza, Madee na Shemeji walikuwa pembeni
Kaka umekiona kitu cha Rav 4?

Jamani hakuna mtu hapo nyuma

Nani anasema muziki wa kizazi kipya unakufa. Mboa kwa Tundaman unamlipa mpaka kaamua kuvuta kitu cha Rav 4? Mi nadhani wasanii wenyewe ndiyo wanajimaliza kwa kutojipanga vizuri na wala hawataki kubadilika. Jamani tusiilaumu game ya Bongo Flava, tujilaumu sisi wenyewe kwakutokuwa wabunifu kwani mashabiki kila siku wanahitaji vitu tofauti.

Read More......
Posted in | | 0 Comments »


Usikose kuicheki safu yako ya kijanja, 'MPAKA HOME' ambayo inapatikana ndani ya gazeti la Risasi linalotoka kila siku ya Jumatato. Wiki hii ilimuibukia Msanii Baby Madaha na kupiga naye stori kibao kuhusu maisha yake. Je, unafahamu mrembo huyo zao la BSS anaminya pande zipi, anaishi na nani, anapendelea nini, ana mchumba au yuko singo?. Usikose.

Read More......
Monday, August 10, 2009 Posted in | | 0 Comments »



Hayo ni baadhi ya maswali ambayo nimekuwa nikulizwa na mashabiki wengi hasa wa muziki wa Bongo Flava. Kiukweli sina jibu la uhakika kwasababu sinajawasiliana naye kwa siku kadhaa, ila inawezekana mshikaji wangu Juma Kassim Kiroboto a.k.a Sir Nature na kundi zima la TMK Wanaume Halisi wanajipanga upya kwa ajili ya kutoka kivingine.

Read More......
Posted in | | 0 Comments »



Wewe Mbongo unaweza kuwa daraja la wasanii wawili nchini, kuibuka na tuzo ya kimataifa kwa kuwapa shavu. Nawazungumzia Nicolas Haule a.k.a Black Rhino na kijana Hamis Mwinjuma 'MwanaFA'.
Bila shaka unajua kilichopo kwamba Black na FA wametajwa kuwania tuzo za Channel O 2008-09, kupitia ngoma zao, Black Chata (Rhino) na Naongea na wewe (FA)hivyo unatakiwa kudondosha kura yako kwa wanetu hao.
Black Chata, ametajwa kwenye categories mbili, Video Bora Afrika Mashariki (Most Gifted East Afrika Video) na Video Bora ya Hip Hop (Most Gifted Hip Hop Video).
Naongea na Wewe ya FA na A.Y imetanjwa kwenye vipengele viwili, Video Bora Afrika Mashariki (Most Gifted East Afrika Video) na Wimbo Bora wa Kushirikiana (Most Gifted Group a.k.a Duo).
Utaona kwamba Black na FA wanakamuana pua kwenye category moja ambayo ni Video Bora Afrika Mashariki; lakini siyo ishu, muhimu hapa ni kuleta heshima home.
Unawezaje kupiga kura? Video Bora Afrika Mashariki, kwa Black tuma SMS yenye maneno 13E kwenda namba +27839208400 au FA, unaandika 13B unatuma kwenye nambari +27839208400.
Video Bora ya Hip Hop, unampigia kura Blak kwa kuandika SMS yenye maneno 10F na unaituma kwenda nambari +27839208400, wakati ili FA ashinde Wimbo Bora wa Kushirikiana, unaandika meseji yenye maneno 4E kisha unai-send namba +27839208400. Inawezekana!

Read More......
Posted in | | 0 Comments »


Kwa habari za kijanja zaidi kuhusiana na ishu za mastaa mbalimbali za Bongo, cheki kunako Abby Cool & MC George Over The Weekend inayopatikana ndani ya gazeti lako la Ijumaa Wikienda kila siku ya J'3. Safu hii ni moja ya kazi ninazofanya kwa ajili ya kuipa jamii burudani ya ukweli.

Read More......
Sunday, August 9, 2009 Posted in | | 0 Comments »