riday, August 7, 2009
MKUBWA NA WANAWE KITAANI
Hii ndiyo albamu ya kwake, Said Hassan Fella yenye jina la Mkubwa na wanawe ambayo tayari ipo kitaani kiwa na ngoma zaidi ya 10. Ndani kuna vichwa kibao likiwemo Kundi zima la TMK Wanaume Family, Jay Moe, Bw. Misosi, Alikiba, Tundaman, Kassim, Bashari na wengine kibao nikiwemo mimi ambaye nimefanya Intro na Autro. Kamata kopi yako ili uone vijana walivyopiga kazi, yaani ni zaidi ya albamu.
K-SHER AVUTA NDINGA MPYAAA
Baada ya kupiga mishemishe za kusaka mkwanja kupitia game ya muziki wa kizazi kipya, mwanadafada Khadija Shaaban a.k.a K-Sher hivi sasa
atakuwa adimu kwenye vituo vya madereza tax kama ilivyokuwa zamani na kwenye
daladala ndiyo kabisaaaa!
Iko hivi, binti ambaye ni mwanamuziki bora wa kike
2008-09 kwa mujibu wa Tuzo za Dandu, ametungua ndinga mpya aina ya Toyota Vitz na
akikatiza nalo kitaani utalishuhudia likiwa na rangi nyekundu huku namba zake za
usajili zikisomeka T 771 BBK.
"Nimeipenda sana plate no. yangu, ile BBK ni kirefu
cha Baby Keisha," alisema K-Sher kwa mapozi alipokuwa akipiga stori na blog hii ya kijanja.
Congratulation mama!

HII NI DAR MPAKA MORO, DOM
Baada ya kuangusha shoo kadhaa za utambulisho wa albamu tatu kwa mpigo katika
mikoa ya Rukwa, Mbeya na Iringa, makundi mawili ya muziki wa kizazi kipya, TMK
Wanaume Family na Tip Top Connection yaliyoungana na kupiga kazi pamoja sasa
yanageuzia mashambulizi Morogoro na Dodoma.
Akipiga stori na safu hii memba wa
TMK, Said Juma 'Chege' alisema kuwa mizuka imeshapanda kwa ajili ya kusababisha
Moro ambako zitatambulishwa albamu nne, Mtoto wa Kichaga ya Amani James Temba
ÔMhÕ, Pesa ya Hamad Ally 'Madee', Ripoti Kamili ya Tundaman na Spark bila kuiweka
kando, Mkubwa na Wanawe ya Said Fella 'Mkubwa'.
Chege ambaye amesimama vilivyo
katika wimbo Running Roll ambao amepewa featuring na mwanadada Wahu, alisema kuwa
katika ziara hiyo ambayo wameipa jina la Wanaume Family na Tip Top Kazini Tour,
wakiwa Moro watakamua kwenye Ukumbi wa Bwalo la Umwema na baadaye Uwanja wa
Jamhuri.
"Siku inayofuata tutadondoka Dom ambako nako tutasimamisha mizuka kwenye
Uwanja wa Jamhuri," alisema Chege ambaye katika wimbo huo aliofanya na Wahu,
ameonesha kiwango cha kijanja.

Sunday, August 2, 2009
EXCLUSIVE
Ishu mpya iliyodondoka ndani ya Ebwana Dah hivi punde kutoka kwa wasanii Mwasiti
Almasi na Khadija Shaban 'K-Sher' inasema kwamba, kwa pamoja mabinti hao
wanatarajia kupiga kolabo ya ukweli ili kuwadhihirishia mashabiki wa muziki wa
Bongo Flava kuwa, mademu pia wanapeana mashavu.
"Sitolitaja jina la wimbo hivi sasa, zaidi nawaomba mashabiki wakae tayari
kuipokea kilabo hiyo, ni kazi ya ukweli ambayo haijawahi kutokea hapa Bongo,"
alisema Mwasiti alipokuwa akiangusha stori na blog hii kutopa pande za Arachuga
alipokuwa anampiga tafu K-Sher kwenye utambulisho wa albamu yake aliyoipa jina
lake.
Kazi kwenu wadau wa burudani, kolabo ya ukweli inakuja.

EBONY FM IKO JUU
Kutoka ndani ya studio za Redio Ebony FM iliyopo Iringa Town mchizi anakwenda kwa jina la Edwin Bashir a.k.a Edo ambaye kwa kushirikiana na uongozi mzima wa kituo hicho cha redio walifanikisha shoo ya TMK na Tip Top kupendeza zaidi.
Kwa mujibu wa Meneja wa kundi la TMK Wanaume Family, Said Fella, Edo alipiga promo ya kufa mtu na kufanikisha tour hiyo iwe ya ukweli ndani ya mkoa huo. Big sana wadau wa burudani pande hizo na mikoa mingine kwa ujumla kwa kutoa sapoti ya ukweli kwa wasanii wetu, isiwe redio za Dar tu ndiyo zionekane muhimu zaidi katika kuiinua game nzima ya muziki wa Bongo Flava.

Subscribe to: Posts (Atom)
Sunday, August 9, 2009
Posted in | |
0 Comments »
One Responses to " "