ILI MUZIKI WETU UWEZE KWENDA KIMATAIFA NI LAZIMA TUBADILIKE, SAPOTI YAKO PIA MUHIMU

Kutoka kiwanja leo tunashuka na uhusiano 10 wa kimapenzi wa mastaa mbalimbali ambao ndani ya mwaka huu ulisambaratika kutokana na kuhitilafiana kwasababu kadhaa japokuwa kuna baadhi yao inasemekana wamerudiana hivi karibuni.
50 CENT na Ciara
Mwana Hip Hop, 50 Cent wa Marekani aliripotiwa kuachana na aliyekuwa mchumba wake, Ciara Harrison. Rafiki wa karibu na Ciara aliueleza mtandao mmoja kuwa, mwanadada huyo aliachia uamuzi huo baada ya kugundua kwamba 50 Cent alikuwa hajatulia.
Usher na Tameka
Usher Raymond na Tameka Foster ambao walifunga ndoa ya nguvu na kufanikiwa kupata watoto wawili, siku kadhaa zilizopita waliripotiwa na vyombo mbalimbali vya habari kuachana, kabla ya wao kuweka wazi hadharani.
Licha ya uhusiano huo kuvunjika tangu mwaka jana, Tameka anayeishi Las Vegas hivi karibuni aliiambia Mahakama ya Fulton kuwa, bado anautambua uhusiano wao uliyofikia tamati Juni 6 mwaka huu.
Jon na Kate Gosselin
Muigizaji Kate Gosselin amesema kuwa, alitengana na mumewe tangu miaka miwili iliyopita.
Msanii huyo ambaye ndoa yao ilidumu kwa miaka 10, alikubali kuishi katika maisha ya upweke.
Paris Hilton & Doug Reinhardt Split
Mwanamitindo, Paris Hilton naye amekuwa ni miongoni mwa mastaa waliyokutana na dhahama hiyo mara kibao kwani hivi karibuni alipigana chini na mpenzi wake, Doug Reinhardt.
Kanye West na Amber Rose.
Mwana Hip Hop, Kanye West mara kadhaa naye amekuwa akiripotiwa kuachana na kipenzi chake, Amber Rose.
CAmeron Diaz na Paul Sculfor
Mastaa wengine waliyotajwa kutosana mwaka huu ni Cameron Diaz na Paul Sculfor, ambapo jarida la Uingereza, Grazia limenukuu chanzo kimoja cha wawili hao kumwagana kuwa ni mawasiliano hafifu waliyokuwa nayo.
Jermaine Dupri
Baada ya kudumu kwa muda wa miaka saba, hivi karibuni Janet Jackson na mpenzi wake, Jermaine Dupri wameripotiwa kuachana.
Mastaa wengine ni Britney Spears aliyeachana na Jason Trawick, Joe Jonas naye ameripotiwa kuachana na Camilla Belle. Kwa upande mwingine mwanamuziki Jessica Simpson na Tony Romo uhusiano wao umefikia tamati mapema mwezi huu ikiwa ni siku chache baada ya aliyekuwa mume wake, Jessca, Nick Lachey kuachana pia na mchumba wake, Vanessa Minnillo.

Friday, August 28, 2009 Posted in | | 0 Comments »

One Responses to "MASTAA 10 WALIYOPIGANA CHINI 2009"

Write a comment