"Hivi sasa sina mpenzi, bado nipo nipo sana"
Hii hapa ni Mpaka Home nyingine ya ukweli ambayo itakudondoshea maisha halisi ya msanii Baby Madaha ambaye kimuziki alifahamika kupitia shindano la Bongo Star Search (BSS) 2008, akaendelea kujituma hadi leo hii ambapo ana albamu moja yenye jina la ÔAmoreÕ, akiwa chini ya Kampuni ya Pilipili Entertainment.
Kimaisha binti huyo mrembo kapiga kambi pande za Kinondoni kwa Manyanya, Dar es Salaam akiwa ni mpangaji kunako bonge la nyumba. Ili kujua mengi kuhusu yeye shuka chini ucheki bonge la intavyuu.
Mpaka Home: Inakuwaje Baby, uko mzuka. Ndani ya mjengo huu wa kisasa unaishi na nani?
Madaha: Mimi niko poa. Hapa naishi peke yangu.
Mpaka Home: Ni jitihada zako mwenyewe au kuna mtu anakupa shavu kimtindo?
Madaha: Hakuna mtu yeyote anayenipa shavu zaidi ya Kampuni ya Pilipili ambayo nafanya nayo kazi.
Mpaka Home: Ratiba yako siku zote ikoje?
Madaha: Mara nyingi huwa nawahi sana kuamka, kitu cha kwanza kufanya huwa ni mazoezi ya kukimbia, natoka hapa mpaka beach. Nikirudi naingia bafuni kuoga kisha natafuta kinywaji baridi kama soda au juisi.
Mpaka Home: Kwanini iwe juisi na sio chai?
Madaha: Chai huwa sipendelei kabisa, yaani imenikalia kushoto.
Mpaka Home: Nini unapenda zaidi kufanya unapokuwa nyumbani?
Madaha: Kusikiliza nyimbo zangu na kufanya kazi kwenye kompyuta.
Mpaka Home: Vipi katika mambo ya maakuli, unaingia jikoni au ndio usupa staa?
Madaha: Hata hivi sasa tunapoongea nimebandika nyama jikoni.
Mpaka Home: Unapendelea zaidi kupika msosi gani?
Madaha: Wali, nyama na mbogamboga.
Mpaka Home: Vipi kuhusu kujipodoa, unamaindi?
Madaha: Yaani mimi ndio mama wa mamekapu.
Mpaka Home: Unapendelea mavazi ya aina gani?
Madaha: Napenda shoti pensi, top na jinsi.
Mpaka Home: Nini kiliwahi kukuumiza sana maishani mwako, nini kilichokufurahisha zaidi?
Madaha: Niliumia sana nilipofiwa na baba yangu mzazi, na nilifurahi sana nilipofanikiwa kutoa albamu yangu ya kwanza ya Amore
Mpaka Home: Kitu gani ambacho ni kero kubwa kwako?
Madaha: Majungu ndiyo kero kubwa kwangu.
Mpaka Home: Vipi kuhusu mpenzi, unaye?
Madaha: Hapana, hivi sasa bado nipo nipo sana tu.
Mpaka Home: Nakushukuru sana Baby.
Madaha: Asante sana, karibu tena.
MAANDALIZI YA MKUTANO MKUU CCM YASHIKA KASI
9 hours ago
One Responses to "MPAKA HOME KWA BABY MADAHA"