ILI MUZIKI WETU UWEZE KWENDA KIMATAIFA NI LAZIMA TUBADILIKE, SAPOTI YAKO PIA MUHIMU


Madee
Babu Tale

Inawezekana ishu kubwa iliyopo kunako game ya muziki wa kizazi kipya hivi sasa ni kuendelea kubomoka kwa Kundi la Tip Top Connection, kitu ambacho kimewafanya baadhi ya wadau wa burudani Bongo watutumie meseji nyingi wakitaka kufahamu mdudu gani hasa ambaye anatishia amani ndani ya umoja huo.
Kwa kumbukumbu za ShowBiz, alianza kuchomoka MB Dog huku mkononi akiwa na faili la sababu ikiwemo kuambulia mkwaja kiduchu kwenye mauzo ya albamu yake, akafuatiwa na Deso aliyekuwa akipiga kazi sambamba na Pingu ambaye pia aliitaja sababu kubwa ni kuambulia ankara za kitoto kwenye mauzo ya kazi yao.
Kabla watu hawajasahau, mwezi uliyopita ÔdogoÕ Z-Anto naye alichomoka na kudai kwamba mkataba wake na familia hiyo umeisha hivyo ameamua kugeukia upande mwingine kwa kupiga kazi chini ya uongozi mpya ambao hajautaja hadi hii leo. Vile vile msanii Pingu ambaye alisimama vyema kwenye kolabo ya ngoma ya ÔBinti KiziwiÕ naye ameonesha nia ya kusepa kwani tangu alipochomoka Z-Anto hajawahi kutokea kunako maskani ya umoja huo wala kuambatana kwenye shoo yoyote ya Tip Top.
Hivi juzi msanii Spark aliyesimama vyema kwenye ngoma ya Nipe Ripoti na Tunda aliendelea kuipunguza kasi ngome hiyo kwa kuachia ngazi huku akiwa na sababu kibao, zikiwemo kutofaidika na umoja huo na kwamba ameamua kupiga kazi kivyake kwakuwa uongozi wa Tip Top haukua fea kwa upande wake na anachohangaikia kwa sasa ni safari yake ya muziki baada ya kujitoa kundini humo.
ShowBiz kama mdau namba moja wa burudani za Kibongo, hususan game ya muziki wa kizazi kipya iliamua kuingia mtaani ili kupata ukweli wa yote hayo na nini chanzo za wasanii hao kuendelea kujiengua Tip Top. Kwa kuanza ilipiga stori na msanii Hamad Ally a.k.a Madee ambaye ni memba namba moja wa familia hiyo ili kujua anauzungumziaje mmomonyoko huo.
ÒMimi kama muasisi wa Tip Top Connection ambaye niliitoa Manzese na kuipeleka pande za Kagera wanapoishi viongozi wetu Abdul Bonge na Babu Tale bado sijajua kwanini wasanii hao wanaojitoa, hawataki kunishirikisha mimi kwakuwa wanapokuja mtu wa kwanza kukutana naye ni mimi ambapo baada ya kuwasikiliza nawapeleka kwa uongozi kabla ya kukubaliwa na kufanya kazi.
ÒKwa mfano MB Dog siku ya kwanza kabisa alikuja na Cheleaman nikawasikiliza, baada ya kuona wako fiti nikawapeleka kwa kina Bonge japo baadaye Chelea alijitoa akabaki Dog peke yake ambaye alikuja pale hana kitu lakini alisikika na kuwa na mafanikio, cha ajabu wakati anaamua kujitoa hakutaka hata kuniambia, nikamsikia kupitia vyombo vya habari tu.
ÒVile vile kwa Pingu na Deso ilikuwa hivyo hivyo japo wao hawakupata mafanikio makubwa sana kutokana na albamu yao kufanya vibaya sokoni, lakini walimudu maisha ya kujitegemea kupitia Tip Top. Ukiachia mbali na hao, msanii kama Z-Anto kafanyiwa vitu vingi sana na Tip Top lakini mwisho wa siku hakutaka hata kuniomba ushauri mimi kabla ya kutoka.
ÒKwa upande wa Spark ndiyo usiseme, alikuja pale kupitia mimi nikampeleka kwa Abdul Bonge japokuwa alionesha kumkataa, nikiwa na Babu Tale (Meneja msaidizi) tuimsimamia mpaka akafanikiwa kuwa juu kupitia umoja wetu, lakini nashangaa leo hii anajitoa bila kutaka ushauri wangu mimi kama msanii mwenzake zaidi ya kuulaumu uongozi.
ÒKuhusu hayo yote mimi kama mwana Tip Top halisi napenda kuwashauri wasanii waliopo na waliojitoa kundini kwamba, wasipende kutumia njia hiyo ili kujitangza zaidi kwani kuna wengine huwa wanatoka na kurudi, muziki ni maisha yao wanachotakiwa kufanya ni kuangalia ni kitu gani hasa wanakipata katika sanaa hii, siyo baada ya miaka kadhaa inabaki historia tu kuwa fulani zamani alikuwa msanii bila kuwa na aset yoyote,Ó alisema Madee.
Kwa upande wake meneja msaidizi wa kundi hilo, Babu Tale ambaye ndiye amekuwa akilalamikiwa zaidi alisema kwamba hahitaji kuwazunguzia sana wasanii waliojitoa bali amegundua kwamba kufanya kazi kiushikaji bila kuwa na mikataba ya kueleweka ni tatizo, kitakachofuata hivi sasa ni kujipanga upya kwani anaamini Tip Top haitakufa kwa sababu ya wasanii waliotoka.
ÒUnajua mimi ningeandikishiana mkataba na msanii kama Tunda ningemfunga tu, kwakuwa asingweza kuufuata ndiyo maana nikaamua tufanye kazi kiushikaji, lakini madhara yake tumeyaona na tayari tumejifunza kitu. Siyo kwamba najisikia vibaya wasanii wakijitoa isipokuwa inanikera zaidi pale wanapokwenda kunizungumzia vibaya wakati nimewafanyia mambo mengi ambayo hawakutarajia. Zaidi nawatakia mafanikio mema katika safari ya muziki wao,Ó alisema Babu Tale ambaye pia alimuwakilisha Abdul Bonge.
Je, wewe mdau wa burudani una lolote kuhusiana na ishu hii, tuambie kwa meseji 0715-110 173 ili tuwarushie wahusika.

Friday, August 28, 2009 Posted in | | 0 Comments »

One Responses to "MADEE, BABU TALE NA ISHU MPYA KWA WALIYOJITOA TIP TOP"

Write a comment