ILI MUZIKI WETU UWEZE KWENDA KIMATAIFA NI LAZIMA TUBADILIKE, SAPOTI YAKO PIA MUHIMU



Ngoma ya Hip Hop inayochangamsha masikio kwa sasa, Msela ambayo imegongwa na
machizi wa kitambo kwenye game, Wateule inaweza kuibua maswali hasa kwa upande wa
video.
Iko hivi, ngoma hiyo ambayo imefanywa na wakongwe, Taikun Ally ‘Mox’, Juma
Mchopanga ‘Jay Moe’, Jafari Msham ‘Jafarai’ na Msafiri Kondo ‘Solo Thang’
inasikika kamili ikiwa na verse nne katika audio wakati kwenye video zipo tatu.
Tofauti kubwa ni hii, kwenye audio magalacha hao wamesimama wote, wakati katika
video Solo hayumo, yaani hajauza sura wala sauti yake haisikiki. Why? Jafarai
anajibu: “Ilibidi tufanye hivyo mzee, Solo yupo bize sana kwahiyo tulimkata
kwenye video ili kuiwahi ngoma kabla haijapotea kwenye game.
“Wakati tunafanya video Solo alikuwa anakabiliwa na mitihani, tukaona tumkate kwa
sababu alikuwa bado hajarekodi video na kutuma clip zake tuziunganishe, lakini no
sweti, kuna dude lingine tumelifanya, ‘Mtaani kuna njaa’ humo Solo ataonekana
kideoni.”

Sunday, August 9, 2009 Posted in | | 0 Comments »

One Responses to "SOLO ALIKUWA TAITI NA MITIHANI -JAFARAI"

Write a comment